kumbukumbu ya miaka 3 ya vivian David Tilya

Mpendwa wetu Vivian David Tillya tarehe  21/08/2008 umetimiza miaka 3 tangu ulipotutoka ghafla bila ya neno la kwa heri  katika ajali ya gari mbaya ya barabarani iliyotokea Mbwewe,Jumapili asubuhi  tarehe 21.08.2005 ukiwa njiani kwenda Arusha kuungana na familia katika jubilee  ya ndoa ya wazazi wako.
 Jiachie na kwa niaba ya wafanyakazi wenzako wa  Clouds Fm 88.4,Prime Time Promotions Ltd ikiwemo familia yako,ndugu jamaa na  marafiki zako tunakukumbuka daima kwa wema,ucheshi,huruma heshima,hekima na  busara zako kwa watu wote wakubwa kwa wadogo.
Nafasi yako katika familia na jamii yote bado  iko wazi na mioyoni mwetu umejaa tele. 
 Pumzika kwa amani dada yetu mpendwa  Vivian-AMEN 
No comments:
Post a Comment