Tanzania Nchi ya Pili  Duniani
 Kwa  utozaji Mkubwa wa Kodi Za  
 Mawasiliano..
   Dk.Maua Daftari.
 ---
Tanzania ni nchi ya pili duniani kwa utozaji mkubwa wa kodi za mawasiliano,ambapo inatoza gharama ya asilimia 30 ukilinganisha na Uturuki ambayo ni ya kwanza kwa asilimia 45.Viwango hivyo ni vikubwa,na kwa upande wa hata nchini gharama hizo ni kubwa na zinaonekana kuwafaidisha zaidi kampuni za simu.

Hiyo yote inatokana na nchi kutokuwa na mkongo wake wa  mawasiliano ambayo ungesaidia kupunguza gharama hizo na kuwabana wenye kampuni  za simu ambao hutumia minara yao binafsi.Hivi karibuni Waziri wa Wizara ya  Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Profesa Peter Msolla aliwasilisha bungeni  makadirio ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2008/09 ambayo ilisisitiza pia  ujenzi wa mkongo huo.
  Mkongo wa mawasiliano wa Taifa ambao uko mbioni  kujengwa,utasaidia kupunguza gharama za mawasiliano nchini zinazopanda mara kwa  mara.Profesa Msolla anasema mara ukamilikapo ujenzi huo,itakuwa rahisi kwa  Mamlaka ya mawasiliano kuwa na sababu za kuwabana kampuni binafsi za simu  kupunguza gharama za mawasiliano kuliko ilivyo sasa.Habari hii na Ikunda Erick  
 
No comments:
Post a Comment