fanya kweli ya tanzaniano yaingia sokoni

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wanaounda kundi la Tanzaniano,linalojumuisha wasanii 3 ambao ni Daz Baba,Ally Mbongo pamoja na Lalumba wameikamilisha albamu yao kwanza inayoitwa Fanya kweli.
Albamu hiyo yenye jumla ya nyimbo kumi, imerekodiwa katika studio  tofautitofauti za hapa jijini ili kuinogesha albamu hiyo,akizunguma na Jiachie  leo mchana kiongozi wa kundi hilo Daz Baba amesema kuwa albamu hiyo tayari  imekwishaingia sokoni kwa ajili ya mauzo.
  Daz amezitaja baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo kuwa ni Modo  wa afrika,Demu ni demu,mambo mengi,hawajui,Fanya kweli na  nyinginezo.Aidha amezitaja studio zilizoipika vema albamu hiyo kuwa ni Mj  Records,Sound Crafters pamoja na Mo Records ya jijini Mwanza
  Daz Baba na Lalumba ni baadhi ya wasanii walitikisa mno wakiwa ndani ya  kundi lao la awali lililoitwa Daz Nundaz akiwemo na Ferooz,ambapo kwa sasa kundi  hilo limebaki jina
 
No comments:
Post a Comment