Friday, August 29, 2008

Rais Kikwete atembelea Ofisi za
USAID na USTDA Nchini
Marekani..
Rais Jakaya Kikwete akilakiwa na Mkuu wa kitengo cha elimu cha shirika la misaada ya kimataifa la marekani USAID Dr.Sarah Moten alipotembelea Ofisi hizo jana.katika mkutano wao Dr Moten alitangaza msaada mpya kusaidia ununuzi wa vitabu vya sayansi kwa shule za sekondari nchini wenye thamani ya dola milioni 1.5 za kimarekani,Rais Kikwete yupo nchini Marekani kwa mwalimo Maalum wa Rais George Bush.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh.Bernard Membe(Kulia)na Mkurugenzi wa wakala wa biashara na ushirikiano wa kimataifa wa marekani(USTDA)Mama Leocadia zak wakitia saini mkataba wa makubaliano ambapo wakala huo utaipatia Tanzania kiasi cha dola 600,000 za kimarekani kuisaidia sekta za umeme,mafuta na gesi nchini Tanzania.Rais Kikwete yupo nchini Marekani kwa Mwaliko Maalum wa Rais George Bush.Picha na Freddy Maro/Ikulu

No comments: