Friday, August 22, 2008

Simba wadungwa Jezi
Mpya..
Mwenyekiti wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Simba,Hassan Dalali akiangalia kwa umakini jezi walizokabidhiwa na wadhamini wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara,Vodacom jana kwa ajili ya msimu mpya wa ligi unaoanza leo.Timu zote zilikabidhiwa vifaa na wadhamini hao jana.
---
Pazia la Ligi Kuu soka Tanzania Bara linafunguliwa leo kwa kuchezwa mechi mbili katika viwanja viwili tofauti.Ligi hiyo ambayo ni mara ya pili inafanyika kwa mfumo mpya wa kufuata kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa FIFA,itashirikisha timu 12.Katika Uwanja wa Taifa,timu ngeni iliyopanda msimu huu ya Villa Squard itakuwa mwenyeji wa wakongwe Simba.
Simba ilimaliza ligi ya mwaka jana ikiwa nafasi ya tatu kwa kujikusanyia pointi 42 nyuma ya mabingwa wa ligi hiyo,Yanga kwa pointi saba na nyuma ya Prisons iliyoshika nafasi ya pili kwa pointi tatu.Habari hii na Anastazia Anyimike,Picha na Mrocky

No comments: