Vodacom Miss Tanzania  2008 Nasreem
 akabidhiwa gari  Lake.
  
 Miss Vodacom Tanzania 2008 Nasreem Kalim akiwa ndani ya gari yake  mpya kabisa aliyokabidhiwa rasmi jana asubuhi jijini Dar es Salaam
 Pichani shoto ni mratibu wa shindano la Miss tanzania kutoka  kampuni ya LINO Hashim Lundega akiwa amemshikia maiki miss tanzania 2008 Nasreem  Kalim akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi,Mkurugenzi wa masoko  Vodacom Ephraim Mafuru pamoja Meneja udhamini wa Voda Emillian Rwejuna\----
 jana asubuhi kampuni ya simu ya mikononi iliyodhamini shindano  la miss Tanzania 2008,Vodacom imekabidhi rasmi zawadi ya gari kwa mrembo wa  Vodacom Miss Tanzania 2008 Nasreem Kalim.
 Gari hilo jipya aina ya Suzuki Garnd Vitara lenye thamani ya sh Millioni 42 limekabidhiwa kwa mrembo huyo na meneja na meneja udhamini wa Vodacom Tanzania,Emillian Rwejuna.Makabidhiano hayo yamefanyika leo asubuhi katika ofisi za Vodashop zilizopo mtaa wa samora jijini Dar na kushuhudiwa na maofisa wa Baraza la sanaaa,Kampuni ya LINO ambao ndio wanaadaaji wa shindano hilo,wadau wa sanaa na waandishi wa habari.
Akizungumza muda mfupi baada ya makabidhiano hayo,Rwejuna alisema Vodacom Tanzania,itaendelea kuboresha zawadi kila mwaka kwa washindi na washiriki,amesema kuwa ni matumaini ya Vodacom Tanzania kwamba zawadi hiyo ya gari ambayo amekabidhiwa itasaidia kurahisisha utendaji na shughuli mbalimbali za kijamii za mrembo huyo.
Rwejuna amesema kuwa sehemu wajibu wa Vodacom Miss Tanzania ni kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii,shughuli ambazo kwa kiwango kikubwa zina mlazimu kusafiri,hivyo ni muhimu sana kuhakikisha kwamba Vodacom Miss Tanzania anakuwa na usafiri wa kuaminika
No comments:
Post a Comment