Friday, August 15, 2008

Mtanzania achemsha
Olimpiki...
Khalid Yahya Rushaka of Tanzania swims during a heat of the men\'s 50m freestyle at the Beijing 2008 Olympic Games in the National Aquatics Center,also known as the Water Cube in Beijing,China,Aug. 14,2008.Rushaka clocked 28.50 seconds.
--------------
PAMOJA na kushindwa kufuzu hatua nyingine,Mtanzania Rushaka Yahya Rashid amevunja rekodi yake katika mchezo wa kuogelea na Michezo ya Olimpiki,inayoendelea Beijing.Yahya ambaye amemaliza akiwa wa 84 kati ya waogeleaji 97 ametumia muda wa sekunde 28:63 ikiwa ni sekunde 0.81 ya muda wake na sekunde 7:04 nyuma ya Mfaransa Amaury Leveaux aliyeongoza.
Mchezaji huyo ambaye alifuzu kushiriki michezo hiyo mwaka jana kwenye mashindano ya dunia ya Melbourne,Australia akitumia muda wa sekunde 29:44 na kushinda katika mita 50 freestyle.Yahya alipangwa kundi la tatu pamoja na waogeleaji kutoka nchi za Mali,Shelisheli, Rwanda,Malawi,Guinea,Maldives na Tajikistan.Habari na Nelly Mtema, Beijing

1 comment:

Anonymous said...

watashinda vipi mazoezi madimbwini?