Tuesday, August 12, 2008

Mchungaji Lwakatare afikishwa
Mahakamani kwa tuhuma za
Utapeli...
MCHUNGAJI wa Kanisa la Assembles of God wa eneo la Madizini,Kata ya Boma,Wilayani Morogoro,Israel Lwakatare(63)Pichani.amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Morogoro kujibu tuhuma za kujipatia fedha kiasi cha sh.milioni 38 kwa njia ya udanganyifu.

Fedha hizo ni viingilio vya kujiunga na Chama cha kuweka na kukopa cha Fungamano la Wajasiliamali Tanzania(FWT)kwa wanachama zaidi ya 254.Akisomewa shitaka mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo,Evodia Kyaruzi,Mwendesha Mashitaka wa Polisi,Salehe Kalulu, alisema mnamo Novemba 15,mwaka jana katika ofisi za eneo la Masuka,mtuhumiwa huyo alifanya udanganyifu huo hadi kufikia mwshoni mwa mwezi uliopita na kusababisha mtafaruku kwa wanachama.

Kwa mujibu wa Mwendesha Mashitaka huyo wa Polisi, mtuhumiwa alikamatwa na Polisi siku tisa zilizopita na kufikishwa Mahakamani leo baada ya kundi la wanachama waliolipa vingilio vya uanachama wa kujiunga na SACCOS hiyo na kukunua hisa kubaini kuwa mchungaaji huyo amewatapeli fedha zao.Mchungaji alikanusha shtaka na kurejeshwa rumande kwa kukosa wadhamini.Picha na habari na mdau John Nditi

No comments: