CCM inajichimbia kaburi
-Sumaye

WAZIRI Mkuu mstaafu,Frederick Sumaye (Pichani) ,amekitahadharisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa kinajichimbia kaburi endapo kitaendeleza vitendo vya rushwa kwenye uchaguzi pamoja na ufisadi.
Sumaye alitoa kauli hiyo nzito juzi wakati akihojiwa kwenye kipindi cha ‘Jicho Letu Wiki Hii’, kilichorushwa hewani na kituo cha Radio Clouds cha jijini Dar es Salaam.
Alisema wapo wagombea wa CCM ambao wameingia madarakani kwa rushwa na hali hiyo ikiachwa ni hatari na itakuwa sawa na kukichimbia kaburi chama.
Alisema wapo wagombea wa CCM ambao wameingia madarakani kwa rushwa na hali hiyo ikiachwa ni hatari na itakuwa sawa na kukichimbia kaburi chama.
Aliitaka jamii inayopokea rushwa kutambua kuwa kiongozi anayeingia kwa rushwa,hawezi kuchapa kazi ipasavyo,kwani atakuwa akitamba kwamba uongozi wake umetokana na rushwa.
“Kiongozi wa aina hiyo hawezi kuwa mchapakazi na atakachokifanya kila anapoingia madarakani, kazi yake ni kukusanya hela kwa njia halali na haramu,ili ukifika wakati wa uchaguzi,awanunue wapiga kura.
“Kiongozi wa aina hiyo hawezi kuwa mchapakazi na atakachokifanya kila anapoingia madarakani, kazi yake ni kukusanya hela kwa njia halali na haramu,ili ukifika wakati wa uchaguzi,awanunue wapiga kura.
Kwa hiyo mchezo wake utakuwa hivyo na mwisho wa siku ni sawa na kukichimbia kaburi chama,na hii ni kwa vyama vyote,”alisema Sumaye.Akitolea mfano kwa upande wake,Sumaye alisema amekuwa kiongozi kwa muda mrefu, lakini hajawahi kutoa rushwa kwa mtu yeyote, ili ampigie kura.
“Mimi nimekuwa kiongozi kwa muda mrefu,sijawahi kutoa rushwa kwa mpiga kura,hata wakati wa uchaguzi wa kuwania nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu(NEC),nilikuwa nikiwakuta watu wamekaa vikundi,lakini niliwaambia wazi wazi kuwa siwezi kutoa rushwa,maana lazima niwe kiongozi wa mfano ndani ya chama changu,”alisema Sumaye.
Bofya na Endelea......>>>>>>
No comments:
Post a Comment