Monday, November 24, 2008

wanafunzi ifm wagoma

Kulikuwepo na doria ya polisi kimtindo kulinda usalama chuoni hapo
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamekusanyika huku wakimsikiliza kiongozi wao akizungumza machache leo asubuhi

Baadhi yao wakisikiliza kwa makini







Wanafunzi wa taasisi ya usimamizi wa fedha (IFM) pichani leo asubuhi nao wamegoma kwa madai yao mbalimbali likiwemo suala la kugomea mitihani pamoja na zimwi kubwa linalosumbua vyuo kadhaa hapa bongo ambavyo navyo vimekubwa na mgomo kikiwemo na chuo kikuu cha Mlimani.

Niliongea na mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho alisema kuwa walichongomea ni ratiba ya mitihani yao ilivyokuwa taiti tofauti na miaka ya nyuma na imekuwa ghafla sana,"tulikuwa tunafanya mtihani mmoja kwa siku lakini kwa sasa tumeambiwa tunafanya mitihani mitatu kwa siku,jambo ambalo wanafunzi wote tumelipinga vikali "alisema mwanafunzi huyo aliyekataa kulitaja jina lake.

Wanafunzi hao waliamua kutoka madarasani na wengine waliokuwa wakiendelea kujisomea kuchomolewa na wanafunzi wenzao na madarasa hayo kupigwa kufuli,kutokana na hali hiyo walinzi wa chuo hicho iliwapasa kufanya kazi ya ziada na kuvunja makufuli hayo,habari zinadatisha kuwa mitihani itawekwa darasani mnamo majira ya saa nane mchana hivyo mwanafunzi atakae amua kufanya haya na asiye fanya haya,mitihani ikiisha uongozi wa chuo ndio utabaini ufanye maamuzi gani.Habari zaidi baadae baadae hivi

No comments: