Thursday, November 20, 2008

MATUKIO KATIKA PICHA !!!
Wanafunzi wa DIT nao wakafukuzwa juzi baada ya vyuo Vikuu kadhaa kufanya hivyo.
Wengine walikaa wakiwa wamekata tamaa wasijue cha kufanya!

Wazee wa EAC nao waklikuwa wanaomba dua Mungu awasaidie walipwe mafao yao!

Wananchi wa Tabata Kisiwani nao walikuwa na lao, mwekezaji kawawekea kifusi na hivyo mvua zikinyesha zinajaa nyumbani mwao!


Baadhi ya wastaafu wa iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakiwa kwenye ofisi za manispaa ya Ilala walipokwenda kudai fedha zao Sh. 30,000 walizolipia kiwanja cha kufanyia mikutano Mnazi Mmoja, lakini polisi wanawasumbua kila wanapotaka kukusanyika.



Watoto wa shule za msingi nao wanaandamana kupinga kukosa masomo kutokana na mgomo wa walimu!



Walitembea kilometa nyingi wengine tokea Mbagala. Lakini la kujiuliza mambo haya yote yanatokana na nini Maendeleo ama watu kukata tamaa!? Vitu vyote hivi viometokea juzi tu hatujui leo kuna nini?






No comments: