Tuesday, November 18, 2008

jeetu patel na wenzie watatu wakubaliwa dhamana

Kiasi cha Sh bilioni 11.7 kimetosha kumtoa nje kwa dhamana mtuhumiwa anayedaiwa kuwa kinara wa ufisadi Jeetu Patel (kulia) na wenzake watatu.

Kiasi hicho ni kutokana na wizi wa Sh bilioni 22.7 anazodaiwa mtuhumiwa huyo na wenzake hao kuiibia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutoka katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) kwa kutumia kampuni nne.

Jeetu na wenzake katika kesi zote katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wamekuwa wanawasilisha hati moja yenye kiasi wanachotakiwa kudhaminiwa washitakiwa wote kama ilivyoamuriwa na mahakama.

Jeetu ambaye jina lake kamili ni Jayantkumar Chandubahi Patel katika kesi hizo anashitakiwa kwa pamoja na Devendra Patel, Amit Nandy na Ketan Chohan.

Hati hizo ambazo zimewasilishwa mahakamani hapo zimethibitishwa na wakaguzi wa serikali ambao wamethibitisha kuwa na thamani ya kiasi hicho kwa kila kesi.


Leo washitakiwa hao walikamilisha taratibu za dhamana katika kesi iliyoko mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi Euphemia Mingi. Kwenye kesi hiyo, Jeetu, Nandy na Patel walidhaminiwa baada ya kutoa hati ya mali ya thamani ya Sh bilioni 5.4.

No comments: