Monday, November 24, 2008

Nina mengi ila kwa leo niishie hapo.!

Dear members

Kwanza nampongeza aliyeanzisha huu mjadala. si kwa sababu ni mimi ni mwanasiasa ila kwa sababu mimi ni MTANZANIA ambaye naguswa moja kwa moja na maisha ya kitanzania. Niende kwenye hoja......

Kwanza wote tunakubali kuwa nchi ina matatizo. Kam ndivyo maswali ya kujadili ni haya
1. Kwa nini matatizo yameongezeka kipindi hiki?
2. Kwa nini migomo imeongezeka kipindi hiki?
3. Je JK Kashindwa kazi? au ni watendaji wake?
4. JK anahujumiwa?
5. Je uhuru umeongezeka kupita vipindi vingine?
Mawazo yangu:...... .

Nakiri kwa uwazi kuwa kipindi hiki kimekuwa na matatizo zaidi ya vipindi vyote vilivyopita. japo matatizo hayo hayakuanza kipindi hiki lakini mengi yamechangiwa wa uongozi wa kipindi hiki. kwa mfano. EPA (2005- Mkapa) , Wastaafu (1977 - Nyerere), NMB (2007 - Kikwete) , Waalimu (Nyerere,mwinyi, mkapa, kikwete), Migomo vyuo (Nyerere,mwinyi, mkapa, kikwete), RUSHWA (mf. Nyerere (sina hakika),mwinyi - LOLIONDO/DHAHABU, mkapa-RADA , kikwete-RICHMOND) .

kama kila awamu imekuwa na matatizo ni kwa nini yaongezeke sasa? Jibu ni rahisi
1. Kwanza ni matarajio ya waTZ kwa rais wao. Alikuja na hojaa ya kuyaondoa matatizo yote ya watazanania kwa kauli mbiu (Maisha bora kwa kila mtanzania). Ndio maana sikushangaa 70% ya ushindi. Nakiri kweli JK alikuwa ana mpango wa maisha bora kwa kila mtanzania. Ila ameshindwa. Kwa nini ameshindwa? jibu ni rahisi sana. (Ni marafiki/mtandao plus UNAFIKI wa JK). Dhambi ya mtandao itamtafuna sana. Mi si mtabori ila ni hali halisi. Kumbuka JK amewekwa pale na marafiki. Mkapa/mwinyi waliwekwa pale na mwalimu. Hivyo marafiki wana-expectataion zao ambazo JK hawezi kuzikwepa. nakumbuka speech moja ya mwalimu alisema "..RAIS ambaye hataki kutowaacha marafiki ikilu itamshinda.. ." We mtu anatuibia (RICHMOND) unasema ni ajali ya kisiasa? Mama yangu!!!! My God!!!.

2. Uelewa wa WaTZ umeongezeka. Tukubali, tusikubali. Uelewa wa TZ umeongezeka sana. Hii imechangiwa pia na kukua kwa ICT. Takwimu za simu zinaonyesha kuwa watanzania takriban mil 10 wana simu za mikononi. Je before 2005 walikuwa wangapi? je walikuwa wanazitumiaje? siku hizi broadcast messages zimekuwa nyingi.


nani anapinga? kumbuka broadcast ya LOWASA KUSULUBIWA BUNGENI. nani hakuipata? Hoja ya ufisadi EPA imeanzia kweye internet broadcast. Mjajua waalimu walitumiana msg za kuhamasishana juu ya magomo kupitia sms? Nawapongeza sana makampuni ya simu has TIGO kwa revolution iliyopo. Ukiweka EXTREME/CHIZIKA/ etc kwa nini usimpigie mwenzako kumweleza jinsi unavyonyanyaswa na serikali? kwa nini naye asifanye vivyo hivyo?

Nina mengi ila kwa leo niishie hapo

Best Regards,
Maxmillian Kattikiro.
Mobile: 0713 520 988 OR 0784 520 988
email:
kattymax2001@yahoo.com; kattymax2003@hotnmail.com

Kadidi: Wadau kama ambavyo nimekuwa nikisema, mjumbe hauwawi

No comments: