Thursday, November 13, 2008

mgambo wa jiji kazini
Na Michuzi
roho iliniuma sana kukuta mgambo hawa wa jiji wakisanya biashara ndogondogo za machinga sehemu ya magomeni usalama, dar. nikawa najiuliza hivi hawana kazi ingine zaidi ya hii?
wadau mnasemaji juu ya hili, ukizingatia jiji lina mambo mengi ya kusimamia ikiwa ni pamoja na kugomboa viwanja vya wazi zilivyotekwa na wenye nazo, kupigwa kufuli kwa bustani ya mnazi mmoja garden na mambo mengine ikiwa na kupiga uzio fukwe za bahari ama kukatazwa kufanyia shughuli kama za harusi na kadhalika. hapo sijaongelea usafi kulinganisha na jiji la kigali. hii imekaaje wadau?

No comments: