Thursday, November 13, 2008

Mkataa Asili Yake Ni Mtumwa!


Nimelipenda wazo la uongozi wa shule ya Msingi Kilimani, Sinza la kuwapeleka wanafunzi wao kijiji cha Makumbusho kujifunza kupiga, kuimba na kucheza ngoma za asili. Kuna watoto wengi wanazaliwa na kukulia mijini bila kwenda vijijini kwenye asili ya wazazi wao. Wasipotambulishwa utamaduni wao baadhi yao hukosa mishikio ya kitamaduni katika maisha ya ukubwani. Pichani ni walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kilimani wakicheza ngoma za asili pale kijiji cha Makumbusho jana mchana.

No comments: