Saturday, November 29, 2008

Jasho Linawatoka Mzigo Wende, Basil Mramba....
Aliwaambia- Ndege ya Rais Itanunuliwa, hata kama ikibidi mle nyasi! Pichani ni Iringa Mjini leo asubuhi.
Kutoka kwa Maggid Mjengwa .

Stars Yaibuka Na Ushindi Mkubwa!

Ni wa mabao 3-1 dhidi ya Sudan. Stars sasa inahitaji sare tu ili iweze kusonga mbele na kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wasiocheza nje ya nchi zao zitakazofanyika nchini Ivory Coast. Mechi ya marudiano ni majuma mawili yajayo ambapo Sudan itahitaji ushindi wa 2-0 ili iweze kusonga mbele. Hongera Stars, na Kila la Heri Stars kwa mechi ijayo.
salamu toka peramiho
Kadidi nilikua safarini kidogo mitaa ya Peramiho nikaona nikupatie hii zawadi ya kikwangua anga cha peramiho kilichoanza kukwangua toka mwaka 1943.
i think the Oldest kati ya vikwangua anga vya tanzania.Zawadi hii pia iwafikie wale wote wanaotokea maeneo hayo Mkoani Ruvuma.

Mdau na Mpenzi wa Masnep
Stewart
wajinga ndio waliwao???
Sema Kadidi,Natumai ni mzima wa afya na unaendelea vyema ktk shughuli zako za kila siku. ebwana naomba utoe issue ya moja ktk blog, ambayo ni kuhusu bei kubwa za Internet ambazo zinazotolewa na Internet Providers wa Kitanzania.
Kwa mfano tu angalia bei za Vodacom
/docredir.asp?docid=3430
ambazo ni kubwa sana kulinganisha na soko la dunia, pia angalia TTCL http://www.ttcl.co.tz/Broadband_Pricing.asp#How
ambazo ni karibia mamilioni ya pesa kulinganisha na soko la dunia. angalia sasa na UK virgin media wanatoza si zaidi ya paund 20 ktk packages zao http://allyours.virginmedia.com/websales/service.do?id=2
au angalia BT
bei ni ndogo sana tena sana. Mkuu naomba fuatilia hili swali kwa nguvu zako zote ili Watanzania nao wapate benefit ya kuwa na cheap internet na kwenda na wakati.
Pia kama ikiwezekana uongozi wa hivi vyombo na vinginevyo viweze kutoa kauli kamili kuhusu bei zao zinazo tesa watanzania na kuwafanya kutokwenda na wakati na kupata faida kubwa ambapo ata Serikali hawaliangalii hili swala.
Mdau UK

mramba na yona kuendelea kusota rumande



Wh. Basil Mramba na Daniel Yona wataendelea kusota tena rumande hadi Jumatatu pamoja na mahakama kuu kuwalegezea masharti ya dhamana.Mahakama kuu katika uamuzi wake wa leo, ililegeza sharti la kuwataka washitakiwa hao kutoa fedha taslimu, badala yake ikawapa mbadala wa kuwasilisha hati za mali yenye thamani ya Sh bilioni 2.9 kila mmoja.


Uamuzi wa kuwataka washitakiwa waweke fedha taslimu ulitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Hakimu Hezron Mwankenja. Lakini sharti hilo lililegezwa jana na mahakama hiyo ya juu.Uamuzi huo wa Jaji Njegafibile Mwaikugile licha ya kupokewa kwa furaha na ndugu wa washitakiwa, haukuwasaidia sana kutokana na hati walizokuwa nazo kuonekana kuwa na dosari kadhaa ambazo zilihitaji uthibitisho kutoka kwa mamlaka zingine.

bado linafuka moshi mweusi


Jengo hili bado linafuka moshi mweusi,Wadau wanausubiria moshi mweupe ndio utakaowapa raha na matumaini mapya zaidi.

kumuona fat joe buku kumi na kumi na tano.!


Ebwanaee ngoma imeiva sasa.! Mwanamuziki wa hip hop kotoka Unyamwezini Fat Joe na mwanadafada mwingine machachari sana katika anga za kufoka foka aitwaye Eve E na mwingine wa tatu (jina tega sikio na macho hapa hapa jamvini) wanatua jijini Dar desemba 8 na kuangusha bonge la shoo katika viwanja vya Gymkana ambapo kiingilio kimepangwa kuwa ni kati ya 10,000/= (mapema) na 15,000/=(getini) kwa kila kichwa.
Aidha katika shoo hiyo itakayokuwa ya aina yake na isio na ubaguzi kabisa kwa wasanii wake wa nyumbani,katika kuipamba shoo hiyo atakuwepo mtu mzima Pro Jay,Mangwea,Mr Blue pamoja na Mwana-FA na Ambwene Yesaya a.ka. AY watakaozindua albamu yao kwa pamoja itakayoitwa Habari ndiyo hiyo na wasanii wengine kadha wa kadha.
Wadau goma hilo lishawekwa wazi kila kitu, hivyo si ya kukosa kabisa, achana na suala la kuhadithiwa. ooh alifanya hivi,ooh alikuja na sijuiii niniiii aah haya maswali kama mtoto wa kijanja hupaswi kuuliza kiivyo,muhimu jichange mapema halafu Inawezekana au sio.Pamoja Wanajamvini

Friday, November 28, 2008

vijana wa heizer records
wanao wakilisha new delhi india

hawa ndo vijana wa heizer records.kutoka kushoto tk,dj tinah na ryhmezone.

siku za mwizi zikifika,hazikwepeki.!


"Jamani mwenzenu najuta kwa kipigo,sijui kama ntarudiao ai"! Mtuhumiwa akisikilizia maumivu baada ya kupata kifinyo kutoka kwa watu wenye hasira kali


Hapa mtuhumiwa akionesha baadhi ya vitasa alivyokutwa navyo



"Twende fanya haraka alaa"!
Mtuhumiwa akiburuzwa kupelekwa kituo cha polisi kati baada ya kupata kibano
Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la William Matiku au William Ngabo a.k.a Baba Nyandalo amejikuta akipata kipigo cha nguvu kutoka kwa wakazi/wafanyakazi wa jengo la kitega uchumi a.k.a NIC leo mchana baada ya kutuhimwa kuiba vitasa vya milango ya jengo hilo lenye vikwangua anga 14.Mzee huyo ambaye alieleza kuwa ni mkazi wa Majumba sita -Ukonga aliokolewa na wasamaria wema na kumpeleka kituo cha polisi central.Aidha baadhi ya watu waliokuwepo kwenye tukio hilo walieleza kuwa hiyo ndio tabia yake sugu aliyonayo ya kukwapua vitu vya watu

Thursday, November 27, 2008

Je ni Lazima Magari ya Taka
Yawe Takataka...?



Hivi ni lazima magari ya taka lazima yawe taka taka?Magari ya taka jijini Dar mengi na makuu, mabovu mno na yenye kuharibika mara mara kwa mara.Najaribu kutafatuta kama kuna sheria inayoruhusu magari haya mabovu ambayo kama taratibu zikifuatwa hayapaswi kuwa bara barani,ndio yatumike katika ukusanyaji taka.Picha na Mdau Bernard Rwebangira
kp na busara zake .........

hotuba za mwalimu
mchanga wa muungano wa tanganyika na zanzibar
mwalimu akiwa ziarani ughaibuni


Nukta77 inatuletea sehemu ya tatu na ya mwisho katika mfululizo wa hotuba ya Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyoitoa katika hoteli ya Kilimanjaro (Kempinski) siku ya Jumanne, tarehe 14 Machi 1995.
Sehemu ya kwanza bofya hapa
Sehemu ya pili bofya hapa.
Sehemu ya tatu bofya hapa.
Mdau Subi

Wednesday, November 26, 2008

Kipanya na busara zake...

Si kila mwanamke unayemwona kanenepa eti ana raha, la hasha!


2008-11-23 12:55:00
Na Anti Flora Wingia

Mpenzi msomaji, bado katika safu yetu hii naendeleza misukosuko wanayopata baadhi ya kinamama wanaotishiwa kupokonywa mali zao na waume zao.

Hebu sikia kilio cha mwenzetu huyu aliyenitumia kupitia barua pepe ya safu hii.

Dada Flora, yupo baba mmoja jirani yangu hivi karibuni ametoa mpya ya mwaka pale alipodiriki kutaka kumchoma kisu mkewe kwa madai kwamba amekataa kumpatia hati ya nyumba.

Nyumba hiyo inavyosemekena imejengwa na mwanamama huyo baada ya kugundua mume hana mwelekeo wowote, licha ya kupata pesa nyingi na kuzimalizia kwenye ulevi na anasa za wanawake.

Mambo hayo yalikuwa ni siri ndani ya muda mrefu moyoni mwa mama huyo ambaye kimuonekano ni mcheshi kwa kila mtu na ilikuwa vigumu kwetu sisi majirani kujua kilichokuwa kinaendelea ndani ya familia hiyo.

Mama huyo ni mwajiriwa serikalini na amekuwa na mzigo wa kulea watoto peke yake pasipo msaada wa mume hata pale watoto wanapohitaji kalamu au daftari kwa baba huwa hawapewi.

Baba huyo yuko radhi kwenda kunywa pombe na wanawake wa nje kuliko kuwapatia watoto madaftari na kalamu!

Wakati mwingine anapoishiwa kabisa pesa ya kunywea pombe kujifanya kuwa presha imepanda anahitaji kupelekwa hospitali.

Bila kufikiria mke pesa atapata wapi, humlazimisha ampeleke hospitali kwa lazima tena na matusi juu eti ``mwanamke gani mwenye roho mbaya namna hii, unayeshindwa kunipeleka hospitali wakati naumwa?

Una kazi ya kununua nguo mpya kila siku na kula machipsi huko kazini kwako, ndio maana unanenepeana tu, huna haya wakati nimekondeana?``

Masikini mama wa watu mwili wake ni ile miili inayostahimili matatizo kwani umwonapo amependeza sana.

Hali kadhalika hata wifi na wakwe wamediriki kumsema kwamba ananenepeana wakati kaka yao (ndugu) amekondeana.

Ndugu za mume wamemlazimisha mama huyo kumpa hati ya nyumba mume huyo kwa madai kwamba mwanamke hana ubavu wa kumiliki mali yoyote bali mmiliki hahali wa nyumba ni mwanaume pamoja na kwamba mama ndiye aliyeijenga wakati baba anajichana na makahaba katika kumbi mbalimbali za starehe.

Mama huyo alipolifikisha suala hilo kwenye vikao vya kifamilia ili lijadiliwe alionekana mbaya anayemdhalilisha mumewe kwa madai kwamba hakupaswa kumficha mume wake hati ya nyumba.

Lakini anachodai ni kwamba nyumba amewajengea watoto ili wapate mahali ka kulala na kwa kuwa anamjua mumewe akili zake zilivyo (kwa kuzingatia kwamba nyumba hiyo hakuchangia hata senti tano) hatoona uchungu kuipiga mnada na kuwaacha watoto wakitangatanga.

Kwani baba huyo yeye anachojua ni kuzaa tu kulea kwake mwiko!

Mama alipolazimisha apewe kibali cha kwenda mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake na kumjua mwenye haki, ndugu waliamua kuliingilia kati na kumshauri baba huyo atafute kiwanja kingine wajenge pamoja na mama huyo ili kuondoa mzozo uliopo sasa.

Lakini baba huyo amekuwa kinyume na ushauri wa ndugu wa pande mbili. Yeye ni pombe na yeye, wanawake na yeye na wakati mwingine hudiriki hata kuwabaka wafanyakazi wake wa ndani.

Hata watoto au hata wake za majirani amekuwa akiwazengea bila aibu. Anapokabiliwa na wenye wake hutoa vitisho na kuwatukana.

Mama wa watu mpaka sasa hathubutu hata kuleta mfanyakazi wa ndani kwa kuogopa lawana na aibu kwani mume wake ndio kituko.

Mama huyo bado anahitaji msaada wa kisheria ili aweze kuachana na baba huyo kwani mpaka sasa hivi ndugu wote wa mume wamesusa kuja hata kusalimia pale nyumbani kwa madai kwamba wifi (mkwe) wao ana roho mbaya na anamnyanyasa ndugu yao.

Eti Anti Flora mtu kunyimwa hati ya nyumba na mkewe ambayo hukuitolea jasho ni kosa?

Kama yeye aliona kujenga nyumba ya kuishi ni muhimu kwa nini basi ajenge kwenye mabaa na Guest houses?

Mama huyu anaomba ushauri wako ili aachane naye kwani kuna siku baba huyo atamtoa roho kwa uchu wa mali kwani inavyosemekana hata kitanda na godoro wanalolalia vyote ni mali ya mama.

Asante sana mpenzi msomaji wangu. Wiki moja iliyopita niliandika malalamiko ya msomaji wetu mwingine yanayofanana na haya.

Kwa Pengine leo nikumbushe tena yale niliyomshauri, tena kupitia mwanasheria aliyebobea, Dk.Sengondo Mvungi, Mhadhiri Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 imeainisha wazi namna mgogoro wa aina hiyo unaweza kutatuliwa.

Kulingana na Dk. Mvungi, mali ya mke au mume aliyoichuma wakati kabla ya ndoa, bado inaendelea kuwa ni mali binafsi ya mhusika na siyo vinginevyo.

Mali ambayo sheria inasisitiza kuwa ni halali kwa wote wawili, yaani mke na mume ni ile iliyochumwa kwa pamoja ndani ya ndoa.

Hiyo iwe ni nyumba au mashamba au mali nyingine yoyote iliyopatikana wawili hao wakiwa tayari wameoana, ni sharti wagawane sawa kwa sawa endapo ndoa hiyo itasambaratika.

Ni matarajio yangu kwamba wasomaji wengine wa safu hii watakuwa wameelimika juu ya mgogoro wa aina hiyo.

Hata hivyo, kwa ushauri zaidi, wasiliana na Chama cha Wanasheria Wanawawake Tanzania(TAWLA) ofisi ziko Ilala karibu na Hospitali ya Amana au Chama cha Waandishi Wanawake Tanzania(TAMWA) ofisi ziko Sinza Dar es Salaam.

Kama unalo linalokutatiza kuhusu purukshani za kimaisha usisite kunikandamizia kupitia barua pepe ``mailto:flora.wingia@guardian.co.tz`` flora.wingia@guardian.co.tz
Wasalaam

Orodha ya mawaziri waliowahi kushitakiwa...


2008-11-26 10:21:43
Na Muhibu Said

Jana historia ya mawaziri waliowahi kuitumikia serikali tangu uhuru iliiingia hatua mpya baada ya mawaziri wawili waandamizi wa serikali ya Awamu ya Tatu, Basil Mramba na Daniel Yona kushitakiwa mahakamani kwa makosa ya jinai na kufanya walikwisha kupanda kizimbani kwa makosa hayo kufikia sita.

Mawaziri hao, baadhi walikamatwa na kufikishwa mahakamani wakiwa madarakani na wengine walichukuliwa hatua hizo wakiwa nje ya madaraka.

Wa kwanza kukamatwa na kufikishwa mahakamani, ni aliyekuwa Waziri wa Sheria katika serikali ya Awamu ya Kwanza iliyokuwa chini ya uongozi wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, marehemu Abdallah Fundikira.

Fundikira alifikishwa mahakamani baada ya kutuhumiwa kuhusika na vitendo vya rushwa na alichukuliwa hatua hiyo wakati huo akiwa madarakani katika miaka ya 1960, miaka michache tangu Tanganyika ipate uhuru. Hata hivyo, alishinda kesi.

Mwingine ni Venance Ngulla, aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha katika serikali ya awamu ya pili katika miaka ya 1990.

Ngulla alikamatwa na kufikishwa mahakamani katika miaka ya 1990, baada ya kutuhumiwa kumiliki gari katika njia zinazotatanisha. Hata hivyo, naye alishinda kesi.

Mwingine, ni aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Nalaila Kiula, katika serikali ya awamu ya pili, iliyokuwa chini ya uongozi wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi katika miaka ya 1990.

Kiula alikamatwa na kufikishwa mahakamani wakati wa utawala wa serikali ya Awamu ya Tatu uliokuwa chini ya uongozi wa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, kwa tuhuma za rushwa. Hata hivyo, naye pia alishinda kesi.

Katika miaka ya katikati ya 90, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu katika serikali ya awamu ya pili, Augustine Mrema naye alikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuwatuhumu hadharani baadhi ya viongozi wakuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali kwamba, wamepokea rushwa yenye thamani ya Sh. milioni 900. Hata hivyo, naye alishinda kesi.

  • SOURCE: Nipashe
Kipanya...

Rais Kikwete akutana
na Gaddafi...


Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi katika ikulu ya Tripoli siku za karibuni.Rais Kikwete alifanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini Libya.Picha na Freddy Maro/Ikulu
Arsenal Ndani Ya 16!

Champion League, ni baada ya kuwafunga Dynamo Kiev 1-0. Hata sare ingetosha kwa Arsenal kusonga mbele. Hongereni " The Gunners"! ( Photo Credit: Reuters)

MACHINGA NA MGAMBO

Hawa jamaa mimi nashindwa nani yuko sawa ama nani mjinga, mgambo kila siku wanakamata mali za machinga lakini nao wanaendelea na biashara!

WAAFRIKA BWANA!

If USA was in Africa , today's papers would write something like:...Just look at the headlines...kickers and straps..:
Don't celebrate yet, McCain tells Obama
Concede defeat, Obama urges McCain
20 opposition cadres riot
McCain Demands Vote Recount
Gordon Brown appointed Chief Negotiator btwn Obama and McCain
A government of national unity proposed
Obama to be the Prime Minister, McCain President
Elections Rigged – McCain Charges
The Church declares elections free and fair
McCain pulls out citing violence
Election results for Arizona awaited
Foreign hand suspected
Trucks with suspected ballot papers crosses into USA from Mexico
I will not accept results, McCain tells Obama
Obama is a puppet of Aufhigunistan and Iraq
Official Results To Be Released Next Month ( Zimbabwe Herald)
WE AFRICANS HAVE A LOT TO LEARN!!!!!!!!!!!!!!!
May GOD bless Africa

Salamu kutoka familia ya Baracka Obama


Familia ya Barack Obama inawatumia salamu za msimu wa sikukuu.

Happy Holidays from the Obama Family
Kuona salamu Bofya linki hapo chini:

http://link.brightcove.com/services/link/bcpid353515028/bctid1349141721
Ali kiba arudi tena marekani, aanzia makamuzi oakland, california


kp na busara zake ....
nywelezzzzz
mambo haya yako kwa da'chemi chemponda kule http://swahilitime.blogspot.com/

Tuesday, November 25, 2008

Dk. shein awatembelea wazazi wa pinda
Makamu wa rais Dk. Mohamed Ali Shein na mkewe mama mwanamema Shein wakipiga stori na mzee mizengo pinda na mama pinda walipowatembelea nyumbani kwao mpanda. Dk. shein yuko katika ziara ya kikazi mkoani Rukwa kukagua maendeleo na kuongea na wananchi.
Albino united yaanza kugawa dozi
Msemaji wa Jeshi la Polisi Kamishna Msaidizi Abdalah Msika akikabidh zawadi ya jezi pamoja na mipira kwa timu ya timu Albino United baada ya kuifunga Times FM bao 2-1
Msemaji wa Jeshi la polisi Afande Abdalah Msika akiwa katikati akiwa na timu ya Albino United ambapo timu hiyo iliibuka mshindi kwa kuifunga Times FM mabao mawili kwa moja mashindano hayo yalifanyia katika uwanja TT Sinza Darajani. Afande Mssika alikuwa mgeni rasmi


wah. yona na mramba washindwa masharti ya dhamana, waenda kulala rumande
wah. daniel yonah na basil pesambili mramba wakiwasili mahakama ya kisutu leo
wah. yonah na mramba wakiondoka mahakama ya kisutu kuelekea segerea
msafara wa kupeleka wah. segerea waondoka mkuku mahakamani.

stei tyund fo moo
Picha na msaada kutoka kwa Michuzi!

The Mramba-Yona Case
TWO former senior cabinet ministers appeared before the Kisutu Resident Magistrate’s Court in Dar es Salaam today charged with abuse of office and occasioning loss of over 11bn/- to the government.
They have been remanded for failure to meet bail conditions.

Mramba Basil Pesambili and Daniel Aggrey Ndhira Yona, who were Minister for Finance and Minister for Mineral and Energy, respectively are facing a total of 13 counts. They pleaded "not guilty" before Resident Magistrate Hezron Mwankenja.

Thought they appeared composed on the dock as the prosecution read the charges against them, Yona was sweating profusely and kept wiping his face the whole day. Members of the public booed at them as they were being taken to remand.

The magistrate granted them bail, but on stringent conditions requiring each to deposit cash 3.9bn/- and secure two reliable sureties.

He also ordered them to surrender their passports and restrained them to leave the city without court’s permission.

None of them met the conditions and were ordered to remain in remand until December 5, when their case will be mentioned.

Investigations into the case have not been completed, the prosecution, led by a team of five prosecutors told the court.

They are Principal State Attorney Boniface Stanslaus, Senior State Attorney Frederick Manyanga and three officials from the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB), Hole Joseph, Benn Linkon and Tabu Mzee.

The then ministers, who are defended by advocates Michael Ngalo, Joseph Tadayo, Sam Mapande, Mafuru Mafuru and Elisa Msuya, arrived at the court premises in a PCCB vehicle, Toyota Land cruiser GX registration number T 319 ATD.

They also boarded the same vehicle when were taken to Keko Remand Prison. Their arraignment was witnessed by several people who jammed at the court premises early in the morning after learing that the duo would be brought there to answer criminal charges.

The charges against the two former ministers are not related with the scandal surrounding the External Payment Arrears (EPA) account of the Bank of Tanzania as previouslyassumed by many.

Both accused are facing jointly five charges of abuse of office and one count of occasioning loss to the government, while Mramba alone faces eight similar counts.
It is alleged that the duo committed the offences between 2002 and 2007 at their respective offices.

The prosecution alleged that between August 2002 and May 28, 2005, being employed in public service and serving as ministers, the duo abused the authority of their offices by doing several decisions.

They include arbitrarily procured M/S Alex Stewart (Assayers) UK and its subsidiary company, M/S Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation to sign and execute gold production assaying agreement in Tanzania in contravention of Public Procurement Act and Mining Act, respectively.

The prosecution alleged that the former ministers left the Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation to sign an addendum extending gold production assaying agreement for two years from June 14, 2005 to June 23, 2007 in contravention of the said Acts.

It is alleged further that the duo invited Dr. Enrique Sugura of the said company to formalise the two years extension before the Government Negotiation Team was convened to work on the matter.

The accused also abstained from attending the mining assayer’s fees issue and submitting the agreement to the Attorney General for vetting as it was recommended by the team consequent upon which act an addendum extending the gold production assaying agreement for two years.

Between June 1003 and May 28, 2005, serving as ministers, willfully and by their failure to take reasonable care or discharge their duties in reasonable manner, the duo unjustifiably allegedly processed a gold production assaying agreement with a clause number 4.3.1.

The prosecution alleged that the said clause led to unjustified tax exemption in favour of M/S Alex Stewart) Assayers) Government Business Corporation, thereby occasioning loss to the government to the tune of 11,752,350,148/-.

While Mramba alone, the prosecution alleged, between October 10, 2004 and November 15, 2005, as Minister for Finance, abused the authority of his office by arbitrarily doing several unjustified decisions.

They include ignoring the recommendation by the Tanzania Revenue Authority (TRA) not to grant tax exemption to M/S Alex Stewart Assayers) Government Business Corporation.

He also allegedly processed and issued Government Notices (GN) No. 423/2003, 424/2003, 497/2004, 498/2004, 377/2005,378/2005, which granted tax exemption to the whole of withholding income tax payable by the said company contrary to the recommendations given by the TRA.

Between 2003 and 2007 in the city, as Minister for Finance, willfully and by his failure to take reasonable care of to discharge his duties in a reasonable manner, Mramba unjustifiably allegedly signed the said government notices.

The said notices, according to the prosecution, had the effect of exempting the said company from paying income tax, thereby occasioning loss to the government of the said 11bn/-.
ze original comedy watinga mahakamani kisutu kurekodi kipindi
wasanii wa ze original comedy wakicheza kama watuhumiwa wa ufisadi nje ya mahakama ya hakimu mkazi ya kisutu wakati kesi ya wah. yona na mramba ikisomwa ndani. inasemekana kipindi hicho kitarushwa alhamisi hii kuanzia saa moja jioni kama kawaida yao
Mapenzi: Kwenye Raha Na Shida!


Picha hii niliipiga jana mchana kule Mufindi. Kuna kisa cha Bwana tajiri sana aliyefunga ndoa na mwanamke masikini. Kabla ya kufunga ndoa bwana yule aliweka sharti moja; kuwa mkewe asimwingile kwa jambo lolote. Atakachosema mume ndicho hicho hicho. Siku mke akivunja sharti hilo, basi, apewe talaka, aondoke nyumbani kwa mume akiwa amechagua moja ya mali za mume huyo. Mali ya kuondoka nayo au kuimiliki, kama ni nyumba, gari, dhahabu au shamba kubwa.

Ndani ya ndoa yao ikatokea siku moja mke yule akamkatisha mumewe katikakati ya mazungumzo. Mke alipinga hoja ya mume. Bwana yule akakasirika sana kwa mkewe kuvunja makubaliano. Akamwambia; " Unakumbuka sharti la ndoa yetu, umelivunja, fikiri sasa ni nini utachukua. Kitu kimoja kati ya mali zangu zote. Kesho asubuhi ikifika unaniambie nikupe na wende nacho kwenu.

Baada ya kauli hiyo, bwana yule kwa hasira hakutaka tena kuongea neno lolote na mkewe. Akanywa kinywaji chake kikali, akalewa na kulala kwenye sofa. Mkewe akawaomba vijana wa jirani wamsaidie kumbeba mumewe.

Alfajiri ilipofika bwana yule akajikuta ameamka nyumbani kwa wakwe zake. Akamwuliza mkewe kulikoni? Akajibiwa; E Bwana Mpendwa wangu, uliniambia nichague kitu kimoja cha kuondoka nacho kutoka nyumbani kwako, nami nimekuchagua WEWE!".

Tangu hapo bwana yule akajifunza jambo moja kubwa maishani mwake; nguvu ya pendo.

Pichani ni Berndette na Benish, raia wa Ubelgiji wanaofanya kazi Mufindi. Bernadette ameteguka mguu. OBS! Kisa nilichosimulia hakihusiani na wawili hao
Ujumbe Umefika!

Kutoka Mufindi, Iringa.

mambo yameiva.!

Pichani shoto ni waliokuwa mawaziri Daniel Yona pamoja na Basil Mramba walipokuwa mahakama ya kisutu leo mchana jijini Dar.

Mawaziri wawili wa zamani Basil Mramba na Daniel Yona wamepandishwa kizimbani leo mchana mahakama ya kisutu na kusomewa mashitaka yao yapatayo 17 ya matumizi mabaya ya fedha pamoja na madaraka waliokuwa nayo,aidha watuhumiwa hao walipaswa kutoa bilioni 3.9 kesh,wadhamini wawili wa kuaminika pamoja kutoa pasi zao kusafiria na pia wametakiwa kutotoka nje ya Dar ikiwa ni masharti ya kupata dhamana.Kutokana moja ya masharti hayo kuwa magumu watuhumiwa hao wameshindwa kupata dhamana na hivyo kupelekwa rumande mpaka desemba 2.

mdau yuko njia panda tumsaidie.!

Niko njia panda sana kipindi hiki.
ILA NINGEOMBA USITOE JINA AU UTAMBULISHO WANGU KWA HILI.
ASANTE KWA KUTUWAKILISHA MTANDAONI.


Wana jukwaa,ningeomba ushauri wenu.Nimekua na mpenzi wangu kwa zaidi ya miaka miwili ingawa alikua anaishi kwao lkn alikua akija kwangu na hata kushinda au kulala siku zingine.Sasa hivi majuzi mdogo wangu wa kiume alihamia kwangu baada ya chuo chao kufungwa ghafla na hivyo tukawa tukiishi nae.

Tatizo likaanzia hapo siku moja nikarudi nkampa mdogo wangu hela akanunue vitu kwa ajili ya kupika na mpenzi wangu huyu akaanza kulalamika sana mpaka sasa bado hatujapata mwafaka.Zaidi anadai kua kuja kwake kwangu atasitisha kwani inaonekana amekua akikwaza ndugu zangu,na pia anadai kua huyu mdogo wangu hamrespect na pia anaona kama yeye anamzibia uhuru wa kukaa nami kama ndugu yake.

Nilipokaa na mdogo wangu kumwuliza yeye alikana kabisa/katu katu kwamba hana tatizo nae na pia anamheshim sana kama shemeji yake,kumweleza huyu mpenzi wangu akaruka akasema ni mnafiki na wala hamaanishi hivyo,cha ajabu nimemwambia niwakutanishe yeye na mdogo wangu amekataa akisema hawezi kukaa na kubishana shemeji yake yeye atakachokifanya ni kutokuja kwangu.

JE HAPO MIMI NIFANYEJE KWANI NIKO NJIA PANDA,nafikiria niachane nae au la kwani simwelewi ananimaanishia nini.jana nikawa nimempa hatima kua kama hawezi kuishi na ndugu zangu kwa upendo kama anaonipa mimi basi sioni sababu ya kuwa nae akanitumia msg kua NITAFUTE ATAKAE WEZA WAPENDA NDG ZANGU.

Nimekua njia panda kwani kiukweli nlikua na malengo makubwa nae coz NILIMPENDA ila naona nashindwa.Je nifanyeje?
Mdau alie njia panda!!

miriam odemba apongezwa jana usiku


Miriam Odemba akionesha Crown yake original kabisa aliovishwa mara baada ya kuibuka mshindi wa pili katika mashindano ya Miss Earth Air 2008 yaliyofanyika nchini Filpine hivi karibuni
Miriam akiwa na mama yake mzazi katika nyuso za furaha kabisa usiku huu kwenye hafla yake fupi ya kupongezwa kwa kuiletea hsehima kubwa Tanzania

Miriam akiwa amepozi na waheshimiwa usiku wa jana ndani ya hoteli ya New Africa,katika hafla ya kumpongeza mlimbwende huyo.kati ni baba yake mzazi Miriam Odemba pamoja na Prof Philimon Sarungi

Miriam akipongezwa na shangazi yake

"Hongera sana mwanangu kwa kutuletea heshima kubwa Tanzania"!

"Well done Miriam "



Miriam akiwa amepozi na wageni waalikwa mbalimbali ndani ya new africa hotel waliofika kumpongeza

Miriam Odemba akiwashukuru wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo baadhi ya viongozi wa serikali waliofika kwenye hafla yake ya kumpongeza kwa ushindi alioibuka nao

Mama yake mzazi Miriam Odemba akiwashukuru wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo fupi ikiwemo kampuni ya Campass Communication ambayo ilishiriki kwa kiasi kikubwa kumuandaa mlimbwende huyo



Mkurugenzi wa Kampuni ya Campass Communication Maria Sarungi akizungumza mbele ya wageni waalikwa kwenye hafla fupi ya kumpongeza mlimbwende wa Dunia namba 2 Miriam Odemba baada ya kuibuka mshindi wa pili katika mashindano ya miss Earth yaliyofanyika hivi karibuni nchini Ufilipino. Hafla hii imefanyika jana usiku ndani ya hoteli ya New Africa.Maria Sarungi alisema kuwa Odemba bado ana kazi kubwa inamkabiri mbele yake kuhakikisha taji hilo linabaki kwa Tanzania, kama vile haitoshi ameongeza kuwa Odemba pia atashiriki kufanya kazi mbali mbali za kijamii hapa nyumbani na pia desemba 28 atarejea nchini Filpine kuungana na mshindi wa kwanza katika kufanya kazi za kijamii nchini humo.Pia atatembelea nchi mbalimbali ikiwepo Singapore na nyinginezo.Aidha Maria amebainisha kuwa Miriam amepata mkataba wa mwaka mmoja wa kufanya kazi nchini humo

Monday, November 24, 2008

ifm hali bado tete,hakuna muafaka.!


Hakuna aliyethubutu kuingia darasani,walithubutu


Mkuu wa chuo cha IFM Prof Joshua Dolie akizungumza hivi punde na wanafunzi

Kwa habari zilizopatikana hivi punde uongozi wa chuo cha IFM umetoa tamko kuwa Wanafunzi wanaotaka kufanya mitihani waingie darasani na wale ambao hawataki kufanya mitihani watawanyike/waondoke eneo la chuo, wale ambao wako hosteli na hawataki kufanya mitihani wabebe vitu vyao waondoke chuoni hapo.

Lakini wanafunzi hao kwa kuonesha umoja wao wakaanza kumzomea mkuu wa chuo mpaka anaondoka eneo hilo ambalo wanafunzi walikuwa wamekusanyika na hakuna muafaka uliokuwa umepatikana.Kuhusu uongozi wa chuo upande wa wanafunzi wao wametoa tamko la kutoingia madarasani kufanya mitihani mpaka uongozi wa chuo utakapo rekebisha ratiba hiyo ambayo inaonekana kuwachanganya wanafunzi hao.

Wanafunzi hao wakakubaliana kuwa wakae chuoni hapo mpaka majira ya saa kumi ili kuwadhibiti wale watakaoonekana wanasaliti wanafunzi wenzao kwa kuingia madarasani na kufanya mitihani.Uongozi huo wa wanafunzi umewataka wanafunzi wenzao kushinikiza uongozi wa chuo kubadili ratiba hiyo ya mitihani kwa kuendelea na mgomo hapo kesho.

Mpaka kamera ya INAWEZEKAN inatoa eneo la tukio hakuna muafaka uliopatikana baina ya wanafunzi na uongozi wa chuo