
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Jaffarai akizungumza mchana mbele ya waandishi wa habari wa televeisheni ya chanel ten kuhusiana na semina iliofanyika iliohusu masuala mbalimbali yakiwemo ya hakimiliki, aidha Jaffarai amesema kuwa semina hiyo imewapa mwanga kiasi wa kuyajua baadhi ya mambo ambayo walikuwa hawajui, kuhusu hakimiliki, Mbali ya hilo Jaffarai amewatupia lawama baadhi ya wasanii ambao hawakujitokeza kwenye semina hiyo iliyokuwa na umuhimu mkubwa kwa wadau wa muziki"Wasanii wengi hawajaja, hata wale wanaojiita masupastaa hajatokea pia, hili ni tatizo kwetu sisi kama wasanii, kwani mwisho wa siku tunakuwa wepesi wa kutoa lawama kwa wahusika, lakini kumbe tatizo bado lipo kwetu sisi wenyewe wasanii"alifafanua Jaffarai
No comments:
Post a Comment