
Pichani kushoto ni Afisa Mtendaji wa chama cha hakimiliki nchini (COSOTA) Bw.Yustus Mkinga akizungumza na wadau mbalimbali wa tasnia ya muziki mchana siku za karibuni kwenye ukumbi wa utamaduni wa russian culture jijini Dar,Semina hiyo iliohusu masuala mbalimbali ikiwemo suala la hakimiliki na athari zake kwenye tasnia ya muziki,utandawazi na athari zake kwenye tasnia ya muziki, ushindani katika tasnia ya muziki na namna ya kuboresha matamasha na muziki Afrika Mashariki na mengineyo,kati ni muwakilishi kutoka Baraza la Sanaa la Taifa kitengo cha idara ya muziki Bw. Ruyembe Mulimba pamoja na Afisa utamaduni na sanaa kutoka Wizara ya habari Utamaduni na Michezo Bw. Michael Kagondela
Aidha Bw Mkinga katika mazungumzo yake aliipongeza kampuni ya Prime Time Promotions na Clouds Fm kwa ujumla kwa kuandaa semina hiyo iliokuwa na manufaa makubwa kwa wadau wote wa muziki, amesema kuwa pamoja na washiriki kujitokeza wachache wasikate tamaa, kwani huo ndio mwanzo.Bw Mkinga amesema pia chama chake kimekuwa kikitupiwa lawama nyingi ikiwemo na kutofanya kazi kiufasaha na kwamba kipo tu ili mradi kipo, jambo ambalo Bw Mkinga alilipinga vikali na kusema kuwa chama hicho kinajitahidi sana kwa kila namna lakini tatizo linakuja kwa baadhi ya wadau wamekuwa hawatoi ushirikiano wa kutosha, matokeo yake wanabakai wanalalama tu.
Bw Mkinga amesema kuwa wasanii wana tatizo kubwa la mikataba ya kazi zao, wengi wao wamekuwa wakiingia mikataba ya usambazaji wa kazi zao kwa wasambazai bila kujua vipengele muhimu, "Wasanii wanapoteza haki zao kwa kutojua thamani ya mikataba ya kazi zao, matokeo yake wanakwenda kwa msambazaji kumpa kazi ya usambazaji wa kazi zake bila mipaka, hawajui kwa kufanya hivyo wanawapa mianya ya kuibiwa zaidi na wasambazaji kila siku, sisi tuna mifano ya mikataba ambayo msanii anatakiwa afahamu kuwa ikoje, tumejaribu kuwaita, baadhi yao wamekuja lakini wnegine ndio hivyo na matokeo yake wanabaki kulalamika kwamba COSOTA haifanyi kazi yake ipasavyo", Kila mmoja akiplay pati yake inavyotakikana basi COSOTA na yenyewe itawajibika vilivyo, hivyo tusikae na kulaumu tu kila mmoja atimize wajibu wake",alisisitiza Bw. Mkinga
No comments:
Post a Comment