
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ajulikanae kwa jina la MB Dog hivi karibuni amekwisha ikamailisha albamu yake ya pili inayoitwa kwa jina la Akili Yangu.Akizungumza na Jiachie leo mchana MB Dog amesema kuwa albamu yake itakuwa na jumla ya nyimbo 10,ambazo amesema zote zipo katika viwango vyenye ubora wa juu tofauti na albamu yake ya awali ilioitwa Si Uliniambia ingawa anaamini nayo ilikuwa na nyimbo nyingi nzuri na zilipendwa sana.
Mb Dog amesema kuwa katika albamu hiyo mpya amewashirikisha wasanii kadhaa wakiwemo nyota, anasema ndani ya albamu hiyo amemshirikisha msanii kutoka Kenya aitwaye Nyota Ndogo,Chid Benz pamoja na kundi la Yakuza Mob,aidha amezitaja baadhi ya nyimbo kadhaa zilizomo kwenye albamu hiyo kuwa ni natamani,akili yangu,rastamani na nyinginezo.Mb Dog kwa sasa tayari amekwisha ikamilisha albamu hiyo na hivi punde itaingia sokoni kwa ajili ya mauzo.
Aidha mpaka sasa Mb Dog ametoa singo yake ya kwanza katika albamu hiyo uitwao natamani ambao umekubalika na kushika chati za vituo vya redio hapa bongo.Akifafanua ni kwa ni albamu hiyo ameamua kuipa jina la Akili yangu, anasema hilo limetokana na yeye kutumia akili nyingi na za kwake katika kuhakikisha albamu yake inakuwa yenye ubora na kiwango cha juu
No comments:
Post a Comment