Thursday, June 12, 2008

Leo ni Siku ya Bajeti..


Pichani ni Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo.
--------------
Bajeti ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2008/09 inatarajiwa kusomwa leo bungeni mjini Dodoma,huku kukiwa na matarajio ya kupunguzwa kwa mzigo wa kodi katika bidhaa muhimu kama petroli.Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo anatarajiwa kusoma bajeti hiyo kuanzia saa 10.00 jioni sambamba na nchi nyingine za Afrika Mashariki katika kipindi hiki ambacho dunia inalia kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na ya vyakula.


Wakati bajeti inasomwa mwaka jana,bei ya petroli mjini Dar es Salaam na maeneo jirani ilikuwa Sh 1,350 kwa lita lakini hivi sasa ni Sh 1,690, huku dizeli ambayo ilikuwa bei nafuu zaidi ya petroli sasa imefikia Sh 1,895 kwa lita mjini Dar es Salaam na hadi Sh 2,000 kwingineko nchini, hali ambayo imeelezwa kuchangia ongezeko la gharama za maisha na mfumuko wa bei.Habari hii na Stella Nyemenohi na Faraja Mgwabati/TSN

No comments: