SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI KUFUATIA AJALI YA HELIKOPTA ILIYOTOKEA TAREHE 9 JUNI, 2008
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametumia salamu za rambirambi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange kufuatia kifo cha watu sita, wakiwemo marubani wawili, mafundi wawili na abiria wawili waliofariki tarehe 9 Juni, 2008 baada ya helikopta waliyokuwa wakisafiria kutoka Arusha kwenda Dar es Salaam kuanguka katika eneo la Oljoro mkoani Arusha
“Nimesikitishwa sana na vifo hivyo vya askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ambao walitoa mchango mkubwa sana wa kuhakikisha kuwa ulinzi na usalama unadumishwa wakati wa mkutano wa Leon H. Sullivan na hivyo kufanikisha na kuiletea nchi heshima”, amesema na kuongeza “Kwa kweli tumepoteza wazalendo na wachapa kazi hodari, natoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo,” Ameongeza.
No comments:
Post a Comment