Friday, June 13, 2008

Rais Kikwete aapisha Majaji wanawake 11

Pichani ni Rais Jakaya Kikwete,akiwa na Majaji wanawake katika picha ya pamoja baada ya kuwaapisha majaji 11 na Msajali wa Mahakama ya Rufani Ikulu jijini Dar es Salaam juzi Ikulu Jijini Dar es salaam.Wengine pichani ni viongozi wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) .
----------
RAIS Jakaya Kikwete amesema uteuzi wake wa majaji wengi wanawake Mahakama Kuu kumetokana na ukweli kuwa, wanawake wanaweza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi.Aliyasema hayo Ikulu Dar es Salaam jana muda mfupi baada ya kuwaapisha majaji 11 wa Mahakama Kuu wakiwamo saba wanawake.
Majaji hao wapya wanawake ni Sophia Wambura,Crecensia Makuru,Rose Temba,Atuganile Ngwala,Rehema Mkuye,Upendo Msuya,na Zainab Muruke.Wengine walioapishwa jana kuwa majaji wa Mahakama Kuu ni Gabriel Rwakibalira,Lawrance Kaduri,Ibrahim Mipawa, na Kassim Nyangarika.Majaji wapya wanawake walimshukuru Rais Kikwete kwa kutambua uwezo wao na kuwapa nafasi.
Jaji Mkuu,Augustino Ramadhani aliwaeleza waandishi wa habari kuwa, majaji ni wachache kulinganisha na mahitaji na kwamba,lengo ni kuwa na Mahakama Kuu katika kila mkoa na kila Mahakama iwe na majaji mawili.Jaji Ramadhani alisema ufinyu wa bajeti ni sababu kubwa ya kuwa na majaji wachache na kwamba Dar es Salaam inahitaji majaji wengi zaidi kwa sababu ya kuwapo kwa vitengo vya ardhi,biashara na kazi katika Mahakama Kuu.Hadi mwisho wa Aprili mwaka huu, kulikuwa na majaji 50 wa Mahakama Kuu Tanzania, 15 kati ya hao walikuwa wanawake hivyo majaji wanawake katika Mahakama hiyo sasa ni 22.

2 comments:

Anonymous said...

It could challenge the ideas of the people who visit your blog.

Anonymous said...

Concentrate to the things that could give information to the people.