Thursday, June 5, 2008
Obasanjo anguruma Sullivan....
Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo,akiteta na Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano wa Leon Sullivan,Andrew Young kwenye mkutano wa nane wa Leon Sullivan mjini Arusha,Katika Mkutano huo Obasanjo ametaka kuwepo na mabadiliko ya riba za kibenki kama Afrika inataka kuinua kilimo chake.
Amesema katika kiwango cha Tanzania ambapo riba za kibenki ni zaidi ya asilimia 18 hakuwezi kuwapo mapinduzi ya kilimo.Rais huyo mstaafu alikuwa akichangia mada juu ya Uwekezaji katika kilimo katika mkutano wa nane wa Sullivan.
“Nimesikia mtu hapa anasema Tanzania riba ni asilimia 18...ni kweli huwezi kukuza kilimo kwa riba hiyo,nchini kwangu (Nigeria) kilimo tumekuza kwa asilimia nne na hata Marekani yenyewe wamekuza kilimo chao kwa asilimia mbili sasa nyinyi kwa asilimia 18 mtakikuza vipi... labda waende wakalime kokeni (mihadarati) ”alisema Obasanjo.Picha na Athumani Hamisi TSN/Arusha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment