Serikali imepanga kupata mapato ya jumla ya shilingi bilioni 7,216.130. Kati ya kiasi hicho, mapato ya ndani ni Shilingi bilioni 4, 728.595 na mapato kutoka kwa wahisani ni shilingi bilioni 2,429.535. Aidha, Serikali inategemea kupata shilingi bilioni 58.000 kutokana na uuzaji wa hisa zake asilimia 21 katika benki ya NMB.
Na katika mwaka 2008/09, matumizi ya Serikali yatakuwa shilingi bilioni 7,216.130. Matumizi ya kawaida yatakuwa shilingi bilioni 4,726.650 ambayo ni chini ya mapato ya ndani ya shilingi bilioni 4,728.595. Matumizi ya maendeleo yatakuwa shilingi bilioni 2,489,480.
Katika matumizi ya maendeleo, kiasi cha shilingi bilioni 1,551.100 kitatokana na fedha za wahisani kupitia miradi pamoja na basketi. Kiasi kilichobaki cha shilingi bilioni 938.380 kitatokana na mchango wa wahisani kupitia misaada ya kibajeti, mapato yatakayotokana na mauzo ya hisa za Serikali pamoja na ziada itakayotokana na mapato ya ndani.
No comments:
Post a Comment