
Moja ya kifaa cha kuzimia moto kikiwa kimeachwa hovyo nje ya jengo la Kitega uchumi a.k.a NIC lililopo mtaa wa Samora , ninavyojua chombo kama hiki pia kina umuhimu wake katika suala zima la kupapambana na moto,Pia lazima kiwe na mchanga ndani ama chochote kile ili hata moto ukitokea kiwe tayari kutoa msaada wa haraka kwa hatua ya awali katika kuzima moto, lakini hiki kiko empty kabisa, halafu unajua nini jengo hili lina historia mbaya sana kwa suala la moto.Kwa hivyo ni vyema wahusika wa jengo hili wakawa makini na utunzaji wa vitu/vifaa vya kuzimia moto kama hivi kwa sababu wanaijua vyema historia ya moto kwa jengo hili.
No comments:
Post a Comment