Thursday, August 14, 2008

rai juu ya rasilimali ya wanyama pori
Tanzania ni nchi iliyobahatika kuwa na rasilimali ya wanayama wa pori ,ambao wanaishi kwenye mazingira yao wenyewe,kwa kimombo natural habitat.Sasa kinachosikitisha ni kwamba hao wananyama wanashambuliwa na maadui wengi nao ni :--
Wanyama wenyewe kwa wenyewe[predation]
- Ujenzi wa hoteli nyingi na kubwa kwenye mji wa wanyama pori[ National parks]
-Uwindaji wa kisasa [professional hunting] au kuua wanyama kwa mchezo[kill for fun]
-Badiliko la Hali ya hewa na ongezeko la joto duniaani[Climate Change and Global wa Warming].
Kweli Tanzania tunaelekea wapi?.Tunajua tuna wanayama wanagapi wa pori?.unajua kama wanayama uonekana wengi sehemu fulani na msimu fulani ni kutokana na kufuata chakula na maji?.
Tanzania ilikuwapo moja ya nchi yenye faru wengi hapa duniani.Sasa kwa nini hawapo tena mpaka tunaletewa mbegu kutoka south africa.
Naomba wachumi wenye uchungu wa nchi wasaidie kuelekeza na kufafanua kuhusu lipo bora kati ya kuwinda,kuuza ,kuua kwa mchezo na watalii waje na kuona wanayama na kuacha pesa zao hapa na kurudi kwao.
Kutokana na Balaa hili la ongezeko la joto na badiliko la hali ya hewa,uchumi wa nchi unategemewa kuadhirika kwa kiasi kikubwa sana kwani wanyama wengi hawataweza kubadilika au kuzoea hali ya hewa mpya[global warming].
Kuna dalili kuwa kuna wanyama wataweza kuhimili au wengine watakufa , au kukimbilia NORTH POLE AU SOUTH POLE.[Hali ya baridi kidogo].
Mbuga zetu zinategemewa kubadilika na kuwa miji mikubwa ,hii ni kutokana na ujenzi wa mahoteli ya kitalii husiokuwa wa busara ndani ya mbuga zetu.Sio muda mrefu tutakuwa na mji mkubwa unaoitwa serengeti na hatujui wanayama watakuwa wamekwenda wapi?.au kufa au kuikimbilia nchi jirani.
Tuiache na kuiboresha rasimali hii kama tulivyoiridhi kutoka kwa wazee wetu wenye busara waliopita.
ASANTENI MUNGU
IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.
The Institute Of Research And Environmental Quality[Ireq]
P.BOX 80259
DAR ES SALAAM
TANZANIA
[EAST AFRICA]
Tell 011 255 755 901002

No comments: