Naunda Tume Haraka Kujua
Chanzo -Prof Mwakyusa..
---------
Wizara ya Afya na ustawi wa Jamii Profesa Mwandosya amesema kwamba ataunda tume kujua kulikuwa na tatizo gani mpaka maafa yakaikumba Muhimbili kwa mgonjwa wa akili,David Donge kushambulia wagonjwa wenzake na kuua wawili.
Mgonjwa huo aliyelazwa na wenzake leo alifikishwa mahakamani kujibu shtaka la mauaji.
Tangazo la kuunda tume amelitoa baada ya kuwatembelea wagonjwa wanaotibiwa majeraha wadi ya Kibasila namba 13.
Wagonjwa hao ni Maurice Oyana(20)na Peter Milanzi (20)wagonjwa wengine Hamis Mohammed(41)na Athuman Abdallah(23)walilazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi(ICU) katika Taasisi ya Mifupa (MOI)katika hospitali hiyo na hali zao si nzuri.Akizungumza baada ya kutembelea wagonjwa hao,Waziri Mwakyusa alisema amezungumza na uongozi wa hospitali hiyo katika vitengo vyote na kupata maelezo kuhusiana na tukio hilo,lakini kutokana na uzito wa tukio lenyewe,imemlazimu kuunda tume.Picha na Mdau Athuman Hamisi/Habari hii na Mdau Msimbe Lukwangule.
No comments:
Post a Comment