Tuesday, August 5, 2008

Makala Ya Leo..
*Wakazi wa Jimbo la Bumbuli wajivunia kilimo
cha chai...
Jimbo la Bumbuli lipo katika milima mirefu ya Usambara.Ni jimbo lenye mandhari safi ya kuvutia,kutokana na kuzungukwa na milima kila kona na misitu ya asili.Milima ya Usambara huvutia kila msafiri aendae nchi jirani za Kenya na Uganda na mikoa ya Arusha,Kilimanjaro, Manyara na Mara.
Maeneo yake mengi yamejaa misitu minene ya kitropiki,yenye ndege, wanyama,mimea na maua adimu nchini.Ni jimbo baridi mwaka mzima.Wakoloni walipenda kuishi huko,hasa nyakati za kiangazi.

No comments: