Saturday, August 9, 2008

Blog Maalum Ya Maombi..

Wadau Dada Mary Damia anawakaribisha wadau wote kwenye Blog maalum ya mambo na ushuhuda mbalimbali kupitia neno la mungu inayokwenda kwa jina la Strictly Gospel
picha chini ni mmoja kati ya wadau mbalimbali wakitoa ushuhuda wao kupitia blog hiyo. unaweza kuitembelea kwa kubofya Hapa
--------------
Bwana Asifiwe watumishi wa Mungu napenda kuwashukuru kwa maombi yenu niliyotuma kwa ajili ya mahitaji yangu ikiwemo suala la kazi,namshukuru Mungu amesikia maombi yenu nimepata ile niliyoiomba.Napenda kutoa shuhuda kwamba nimepata kazi nzuri sana,Mungu azidi kuwatia nguvu wote mnaotuombea pia ningependa kuwashauri watu wote wenye mahitaji mbalimbali wayalete kwenye blog hakika watamuona Mungu kwani maombi yawengi yana nguvu sana sina chakumpa Mungu zaidi yakumrudisha sifa na Utukufu kwake naomba mniombee nikawe muadilifu,mwaminifu na mchapa kazi pia muifunike kazi yangu kwa damu ya Yesu.
Mungu awe nanyi.
—-Cossy Dezy—-

No comments: