Friday, June 13, 2008

TAARIFA YA KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU OMARY JAFFARI NGWAYA ..

MWILI WA MAREHEMU UTAFIKA DAR-ES-SALAAM SIKU YA JUMATATU SAA MBILI USIKU NA HII NDIO RATIBA KAMILI.
Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Italy unapenda kukutaarifu kuwa mipango yote ya kusafirisha mwili wa marehemu mtajwa hapo juu imekamilika
jana saa 10:00 tarehe 12/06/2008 Watanzania walikusanyika kwenda kutoa heshima na kuuaga mwili wa marehemu.
Mwili wa marehemu unatarajia kuondoka siku ya Jumamosi tarehe 14/06/2008 kutokea ROMA na ndege ya shirika la SWISS namba :
LX1733 saa 19:50 na kufika ZURICH saa 21:30.
Mwili utaondoka tena Zurich siku ya jumatatu tarehe 16/06/2008 na ndege ya shirika la SWISS NAMBA:
LX292 Saa 09:35hr na kufika DAR-ES- SALAAM TANZANIA saa 20:10 hrs.
KWA TAARIFA ZA MAZIKO HUKO NYUMBANI PIGA SIMU NAMBA :
CELL. 0717 683912

No comments: