Saturday, June 14, 2008

Penye malengo hapakosi mafanikio.

Makala na Dismas Lyassa

Kuna watu wengi wamekuwa wakikata tamaa pale wanapoona mambo

yao hayaendi vizuri. Lakini ukweli ni kwamba kukata tamaa ni tabia

isiyofaa kuendelezwa, ni tabia hatarishi kwa maisha yako na unapaswa

kuachana nayo.

Hata kama mambo yanakuwa magumu kiasi gani, jipe moyo

kwamba uko kwenye mapito na ipo siku mambo yatakuwa

safi, utakuwa bora.

Hata kama labda wazazi wako hawakupendi, au labda

umezaliwa hujui mzazi hata mmoja, au labda baba au

mama yako amekutelekeza, huna sababu ya kukata tamaa

kwa sababu wapo watu wamekuwa na maisha mazuri hata

kama hawakuwa na wazazi.

Msingi wa kuwa na maisha bora sio kuwa na wazazi.

Waulize watu wengi waliofanikiwa watakuambia hili

ninalokueleza kwamba walifanikiwa kwa jitihada zao na

wakati mwingine kwa msaada wa watu ambao hata

hawakuwategemea.

Jambo la msingi kwako ni kuhakikisha unakuwa na

malengo, usiishi tu ili mradi siku zinakwenda mbele.

Sema nataka kuwa kama fulani, nataka kuwa fulani,

kisha omba ushauri kwa watu ambao unafikiri wanaweza

kukupa mawazo mazuri.

Wakati fulani mwaka 2001 kulikuwa na kijana nakumbuka


alikuja kwangu akaniambia, nimezaliwa


Sijui baba wala mama, ninalelewa na bibi, nisaidie


nawezaje kuwa na maisha


bora.

Wakati huo alikuwa akiishi chumba ambacho ndani yake

walikuwa wakilala watu zaidi ya watatu. Nilimueleza

jambo la kufanya, kwamba vyovyote itakavyokuwa ni

vizuri kutafuta chumba chake cha kuishi.

Kweli baada ya muda alifanya hivyo. Baadaye nilimueleza

kwamba atafute kiwanja ajenge nyumba yake, akasema

fedha nitapata wapi, nikamjibu kwani unajua viwanja

wanauza shilingi ngapi, akasema sijui.

Kwa bahati nzuri nilimjua mzee mmoja aliyekuwa akiuza

kiwanja chake, alikuwa tayari hata kulipwa kidogo

kidogo. Alibahatika akanunua, hivyo ninavyokwambia

tayari ana nyumba nzuri kubwa.

Ndugu yangu ninachotaka kukwambia ni kwamba kuna watu

wamekuwa wakisema haiwezekani kufanya jambo fulani,

hata kabla ya kulijua jambo hilo. Mwingine kama huyu

anasema hai­wezekani kununua kiwanja kwa sababu ni bei

ya juu, wakati kumbe kuna watu wanauza viwanja na

ukalipia kidogo kidogo.

Ndugu ni vizuri kabla ya kusema jambo fulani

haliwezekani, ukalifanyia uchunguzi jambo hilo na

kupata jibu la uhakika. Hata kama kwa mfano unataka

kununua gari, usilalamike kwamba magari yanauzwa bei

mbaya, badala yake tembelea kwenye maeneo wanayouza

magari, ona bei zake..

Kuna watu wanauza magari tena kwa bei ya chini, labda

kwa sababu wana


matatizo. Eeeh bwana unaweza kuona mtu mwanae anaumwa


au ana kesi mahakamani, anatakiwa kupata fedha kwa


haraka, yuko tayari kuuza gari au mali yake hata kwa


bei ndogo ili suala lake lipatiwe ufumbuzi.

Ninachosisitiza ni umuhimu wa kutokata tamaa, badala

yake unapokuwa na jambo hakikisha unalitafutia

uvumbuzi. Msingi wa kupata jibu sahihi la jambo

linalokusumbua, sio kukata tamaa, bali kusaka dawa ya

tatizo linalokusumbua.

Yaani kama unaumwa ni kwa kwenda kwa daktari na kupata

tiba, sio kulalamika kwamba aaah Mungu huyu vipi mbona

kila mwaka mimi tu naumwa. Sio kwa kulalamika kwamba

Mungu huyu inakuwaje mbona wengine wana maisha mazuri,

mimi ni hali mbaya.

Ijenge akili yako katika kutatua tatizo, sio kuliona

tatizo kama tatizo. Aidha unatakiwa kuachana na

fikra mbaya.

Jipe moyo kuwa unaweza, kisha tafuta njia ya

kufikia kwenye hali ya mafanikio unayoyaota.

Zaidi ya yote achana na marafiki na watu wote ambao

midomo yao imejaa kauli za kukatisha tamaa, maana wapo

watu wengine utawasikia wakisema "aaah ndugu hilo

huliwezi, wameshindwa watu wenye elimu zaidi yako,

wameshindwa watu wenye fedha zaidi yako, huliwezi hilo


achana nalo".

Penda kuwa na jamaa ambao wanaku-

Tia moyo , badala ya kusema haiwezekani , wanakuambia

njia za kufanya ili hilo jambo liwezekane. Katika maisha

kila jambo linawezekana, jambo la msin­gi ni kujipanga

vizuri, kuangalia nini cha kufanya ili kupata mafanikio.

Hakuna kushindwa.

Aidha kama liko jambo unalijaribu, lakini mara nyingi

unaendelea kulifanya vibaya, usikate tamaa. Jamaa


ambaye
alizindua balbu, alijaribu na kufeli zaidi ya

mara 20, baadaye alifanikiwa.

Kufeli jambo ni kitu cha kawaida, na wala kufeli si

mwisho wa yote. Ukishindwa hiki, jaribu kwa njia

nyingine, hadi uweze kufanikiwa.

Katika maisha ili uweze kuwa mshindi mzuri, ni vizuri

kuacha kuwa muongo. Jitahidi kuwa mwaminifu, utaweza

kuwa na marafiki wengi na hata watu wengi ambao

wanaweza kukusaidia katika siku zako za baadaye.RIDHIKA

NA ULIVYO;Wakati mwingine ni vizuri kujikubali ulivyo,

kuridhika ulivyo. Acha kupendelea kuiga sana wengine.

Anzisha staili yako ya maisha, wengine waige sio lazima

wewe tu uwe unaiga tabia za wengine. Watu wengi

wanaona maisha ni magumu kwa sababu ya tabia yao ya

kujifananisha na; wengine.

Anaona wengine wana magari, na yeye anataka kufanya

mashindano awe na gari la thamani kubwa zaidi, anaona

wengine wana nyumba nzuri, naye anatamani awe na zaidi

ya hiyo ili amuonyeshe kuwa yeye ni zaidi, haya si

maisha mazuri ndugu yangu, anzisha

Staili yako ya maisha, acha kuiga sana staili za

wenzako.

No comments: