
KITENDAWILI kilichotokana na mgongano wa kiuongozi ndani ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), huenda kikapata jibu hivi karibuni kutokana na kurejea nchini kwa Sheikh Mkuu, Mufti Shaaban bin Simba.
Mufti Simba alirejea nchini jana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia, iliyowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro majira ya saa 8 alasiri, akitokea nchini India.
Kwa muda wa miezi kadhaa, Mufti Simba alikuwa India, ambako alilazwa kwa ajili ya matibabu ya kisukari na ugonjwa wa moyo.
Akizungumza baada ya kuwasili, Mufti Simba alisema anamshukuru Mungu kuwa matibabu aliyopatiwa yamemwezesha kupata nafuu na hivyo kuweza kurejea nyumbani.
Akizungumza kwa utulivu, alisema kuwa hivi sasa anajisikia nafuu sana ingawa anatakiwa kurudi tena nchini India kwa ajili ya kufanya vipimo vitakavyowawezesha madaktari wanaomtibu kujua maendeleo ya afya yake.
Mufti Simba, aliyekuwa ameandamana na Kaimu Katibu Mkuu wa BAKWATA, Sheikh Ally Mzee, alisema kuwa anatakiwa kurudi nchini humo baada ya miezi mitatu.
Alisema hivi sasa atakuwa katika mapumziko ya siku kadhaa mjini Arusha, kabla hajarea ofisini kuanza kazi rasmi. Hata hivyo, hakufafanua mapumziko yake yatakuwa ya muda gani.Habari na Ramadhani Siwayombe, Arusha
6 comments:
Well for me its better to be more realistic.
Thanks to the blog owner. What a blog! nice idea.
Well done for this wonderful blog.
Baw ah, kasagad sa imo maghimo blog. Nalingaw gd ko basa.
The nice thing with this blog is, its very awsome when it comes to there topic.
Interesting topics could give you more visitors to your site. So Keep up the good work.
Post a Comment