Wednesday, June 4, 2008

Kocha Maximo na Sare Taifa Stars


Timu yetu ya Taifa imetoka sare na Mauritius juzi.Tumepoteza nafasi nzuri ya kuibuka na ushindi mnono nyumbani. Kocha anaonekana kuridhika na sare hiyo. Juzi hapa tumetoa sare na Malawi kwenye friendly match. Ukiangalia rekodi ya Stars tunaona kuwa sare ni nyingi mno. Hatuwezi kwenda kwenye fainali za Kombe la Dunia kwa kutoka sare! Hata kwenda Angola kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika hakwendeki kwa 'sare'.


Tunatakiwa tushinde mechi nyingi zaidi. Hivi kile kiwango cha Stars cha mwaka jana kimekwenda wapi? Kama tuliweza kumfunga Burkina Faso nyumbani na ugenini na kuwatoa jasho Senegal Mwanza iweje ka-nchi kadogo kimpira kama Mauritius katutoe jasho nyumbani kwetu? Kuna tatizo, kocha Maximo ana lazima ya kufanya mabadiliko ya kimsingi ya kikosi. Nimeona mechi ile kupitia TV. Pale katikati kumepwaya.


Halafu nafasi nyingi zile tulizozipoteza huwa adimu sana kuzipata ukipambana na nchi zilizo bora kimpira. Maximo ainue kamba. Kwa sasa iko chini sana. Mathalan, Ivo Mapunda hachezi kama kipa wa kisasa. Kilio cha wadau kumtaka Kaseja na Mgosi uwanjani nacho kichukuliwe kwa umakini. Zitafutwe mechi ngumu za kirafiki. Wadau wasikilizwe,wasibezwe.Jamani Cameroon wanakujakesho kutwa tu! Cameroon hawamtumi mtoto dukani, kina Etoo wanakuja wenyewe! Taifa Stars ni yetu sote. Tusiogope kujikosoa ili tuwe bora zaidi.

No comments: