Tuesday, June 10, 2008

Helikopta ya JWTZ yaanguka, Yaua 6..


------------
HELKOPTA ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), iliyokuwa inafanya doria wakati wa Mkutano wa Leon H Sullivan katika maeneo mbalimbali ya Arusha imeanguka jana mchana na kuua watu sita, wanne miongoni mwao wakiwa wanajeshi.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Matei Basilio alithitibisha jana kutokea kwa ajali hiyo katika eneo la Matevesi Wilayani Arumeru jirani kidogo na Uwanja Mdogo wa Ndege wa Arusha na kueleza kuwa watu wote sita waliokuwemo kwenye helikopta hiyo wamekufa.

''Ninachoweza kusema sasa ni kweli ajali hiyo imetokea na wote sita wamefariki baada ya helikopta hiyo kuwaka moto baada ya kuanguka,'' alisema Basilio.

Kamanda Basilio alisema kuwa helikopta hiyo ilianguka ikiwa safarini kwenda Dodoma jana baada ya kumaliza kazi maalum ya kuimarisha ulinzi wakati wa mkutano wa Leon H Sullivan.
Hata hivyo, Kamanda Basilio alisema majina ya wanajeshi ni kanali Makele, Meja Sinda, Luteni Kirunga na PT Mambe. Wengine ni mtoto mdogo Diana Mzirai na Irine Jitenga. Miili yote imehifadhiwa chumba cha maiti cha Hospitali ya Mount Meru jijini Arusha.Habari na Juma Musa/Arusha

No comments: