Wednesday, April 23, 2008

Wanafunzi Chuo Kikuu Waandamana..


Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani wakiandamana jana kupinga kusimamishwa masomo kwa wenzao kadhaa kwa tuhuma mbali mbali za utovu wa nidhamu. wanafunzi hawa walitawanywa kwa mabomu na Polisi.Mgomo wa wanafunzi hao ulianza rasmi jana majira ya saa 5:30 asubuhi,ambapo waliandama kutoka hosteli namba saba hadi Ukumbi wa Nkrumah na kuwatoa nje wanafunzi wote waliokuwa wanaendelea na masomo.

Wanafunzi hao waliendelea na utaratibu huo wa kuzunguka katika madarasa mbalimbali ya chuo hicho kwa lengo la kuwatafuta wanzao waliokuwa wanaenandelea na masomo kwa lengo la kuwatoa nje .

Mgomo huo uliambatana na maandamano ya kuzunguka chuo hicho huku wakiimba nyimbo mbalimbali zilizoashiria amani na mshikamano zikiwemo za "Mungu ibariki Tanzania, Tusipowatetea sisi ninani atakaye watetea na wasiporudishwa na sisi tufukuzwe".Habari hii na Jackson Odoyo na Joymertha

No comments: