Thursday, April 24, 2008

Kumekuchaa Mh Kimaro (MB) awasha Moto Bungenii


Mbunge wa Vunjo (CCM) Aloyce Kimaro,akichangia wakati wa mjadala wa muswada wa Nishati na Madini mjini Dodoma.
-----------------

MBUNGE wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM), amewatuhumu Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, mkewe Mama Anna Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona, kuwa walinunua mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira, wilayani Rungwe, Mbeya kwa kificho.

Mbunge huyo alidai bungeni jana kuwa mwaka 2004, Mkapa kwa kushirikiana na mkewe pamoja na Yona, walianzisha Kampuni ya TanPower Resources Ltd na mwaka mmoja baadaye wakauziwa machimbo ya Kiwira kimya kimya.

Kimaro alitoa madai hayo alipokuwa akichangia Muswada wa Sheria ya Umeme wa Mwaka 2008, bungeni,jana.

Alidai kuwa katika mauziano hayo ya siri, Kampuni ya TanPower Resources Limited,

ilikuwa iilipe serikali Sh700milioni katika mradi huo uliogharimu, zaidi ya Sh4bilioni, lakini kampuni hiyo ilifanya malipo ya awali ya Sh70milioni tu.

No comments: