Wednesday, April 30, 2008

mdau atunisha mchango kwa mtoto samweli Nkya !!


samweli

mdau meshack mfugale akabidhi dola 500 kwa emmanuel nkya kama mchango wake kwa mtoto samwel nkya (pichani juu) anayehitaji kwenda india kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji na matibabu katika uso wake ambao umeharibika. walioshuhudia ni wajumbe wa kamati ya kumsaidia mtoto samweli akatibiwe.

mdau mfugale anayefanya kazi darfur, sudan, ni mmoja ya wadau wengi waliojitokeza kumchaangia mtoto huyu kiasi sasa mchango umetimia dola 9,500 na zimebakia dola 2,500 tu kukamilisha matakwa yote ikiwa ni pamoja na tiketi ya ndege mtoto samwel na baba yake, matibabu na malazi hospitali mwezi mmoja.

Baba wa mtoto huyo, emmanuel nkya, ametoa shukrani sana kwa wasamaria wema wote waliochangia kwa hali na mali. safari ya kwenda india inatarajiwa kufanyika wakati wowote kuanzia sasa.

No comments: