Tuesday, April 29, 2008

Undani zaidi Juu ya Kifo Cha Mtoto Salome..


Pichani juu ni kijana Ramadhani Mussa (12)ambae anashikiliwa na polisi Mkoa wa Ilala kwa kukutwa na kichwa cha mtoto mdogo Salome Yohana (3) alichokuwa amekibeba katika mfuko wa rambo kwenye hospital ya taifa ya muhimbili Hivi karibuni.

Picha juu kulia aliposimama Mdau,ni sehemu inayoaminika kuwa mtoto
Salome alichinjwa..
---------
Mauaji ya kikatili ya kuchinjwa kama kuku mtoto pekee kwa wazazi wake, Salome Yohana (3) yameumiza wakazi wengi wa jiji la Dar es Salaam na hata nje ya jiji na vitongoji vyake na wameiomba serikali kuwachukulia hatua kali wote waliohusika na kitendo hicho.
Akimsimulia mwandishi wetu jinsi Salome alivyotoweka nyumbani na kukutwa amechinjwa, mama mzazi wa mtoto huyo, Upendo Dustan (27) alisema kuwa siku hiyo ya Ijumaa wiki iliyopita majira ya saa 2.00 usiku aliandaa chakula wakala na mwanaye ambaye baadaye alikwenda kucheza nje na mtoto wa jirani yao.

No comments: