Tuesday, April 29, 2008

Mafua ya Kuku Janga la Taifa..


Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akishuhudia wakati Kuku akitolewa damu kwa ajili ya kupimwa kama ana maambukizi ya ugonjwa wa mafua makali ya ndege,katika sherehe ya uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Tahadhali na Udhibiti wa ugonjwa huo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana.Kulia ni Dk. Chanasa Mpelumbe-Ngeleja kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kushoto ni,Mfugaji wa Kuku Bi Stella Chambo na katikati ni Waziri wa mifugo na uvuvi Mh John Pombe Magufuli.Picha Ofisi ya Waziri Mkuu
------------
SERIKALI imeutangaza ugonjwa wa mafua ya ndege kuwa ni moja ya majanga ya kitaifa yanayoikabili nchi.
Hayo yalisemwa jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati akizindua mpango tahadhari na udhibiti wa ugonjwa wa mafua ya ndege nchini, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
"Baada ya kutambua tishio la ugonjwa huu ni kubwa na lina athari kubwa, serikali imeamua kutangaza ugonjwa huu ni moja ya majanga ya kitaifa. Kwa maana hiyo serikali imeamua kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na ugonjwa huo," alisisitiza Pinda.
Waziri Mkuu Pinda alisema kuna uwezekano mkubwa wa ugonjwa huo kuingia nchini kwa kuwa tayari umeenea Kusini mwa nchi ya Sudan.Habari hii na James Magai

No comments: