Friday, April 25, 2008

Misa ya Kuiombea nchi Yetu Tanzania Westminster Abbey Uingereza...


Kama mnavyofahamu, tarehe 26 Aprili – Siku Kuu ya Muungano, ndio siku tunayoiadhimisha kama siku ya Taifa letu. Kanisa la Westminster Abbey, London, SW1P 3PA, lina utaratibu wa kusoma Misa kwenye Siku za Mataifa yote yaliyo wanachama wa Jumuiya ya Madola – (Commonwealth). Ni kwa jinsi hiyo, wametualika Watanzania wote, tukahudhurie Misa hiyo waliyoipanga kufanyika siku ya Ijumaa, tarehe 25 Aprili 2008 kwenye Kanisa hilo.

Hivyo basi, Watanzania wote muishio katika eneo hili, tunaombwa kuhudhuria misa hiyo. Wahudhuriaji wote tumeombwa tuwe tumefika Kanisani hapo kabla ya saa 10:45 jioni..

No comments: