Wednesday, April 23, 2008

Mkong'oto....


Pichani baadhi ya wanafunzi walioshiriki mgomo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana wakiwa chini ya ulinzi kwenye gari la kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) ambao jana walitembeza mkong'oto kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliodaiwa kuchochea fujo na kuwahimiza wenzao kugomea masomo chuoni hapo.Wanafunzi hao walipata kipigo hicho jana mchana na kusababisha baadhi yao kuumia na wengine kukamatwa kwa kusababisha fujo chuoni.Kuitwa kwa askari hao kulitokana na wanafunzi hao kuendesha mgomo siku mbili kwa madai ya kutaka wenzao waliosimamishwa masomo warejee chuoni bila masharti.Habari na Pius Rugonzibwa,Picha na Salhim Shao.

No comments: