Tuesday, April 29, 2008

Fichueni Mafisadi -Rais Kikwete


Mkurugenzi wa Mawasiliano na Habari wa Ikulu, Bw Salvator Rweyemamu akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ikulu jana jijini Dar es Salaam juu ya ziara ya Rais Jakaya Kikwete kuelekea nchini Ethiopia na Uganda kutekeleza majukumu yake kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).

katika Mazungumzo hayo na waandishi wa Habari Bw Rweyemamu alisema Rais Jakaya Kikwete amewataka wafanyakazi nchini,kukataa kutumika katika miradi ya mafisadi na vigogo wa rushwa ili kuwafanya vigogo hao washindwe kutimiza malengo yao. alisema badala yake Rais amewataka wafanyakazi kuwa mstari wa mbele katika kuwafichua vigogo hao bila woga.

Alisema iwapo wafanyakazi watagoma kutumikishwa katika `madili` ya kifisadi na rushwa, itakuwa vigumu kwa vinara wa mambo hayo kufanikisha matendo hayo maovu.

Katika kuwapa moyo wafanyakazi hasa wakati huu wanapojiandaa kusherehekea SikuKuu yao ya Mei Mosi, Bw. Rweyemamu alisema Rais Kikwete amefurahishwa mno na kauli mbiu ya mwaka huu inayosema`Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana Mafisadi wakitokomezwa'.Kutokana na hilo,Rais amewataka wafanyakazi wawe mstari wa mbele katika mapambano ya kutokomeza rushwa na ufisadi.

`Rais anawaomba wafanyakazi, viongozi na wananchi kwa ujumla washirikiane na Serikali katika mapambano haya,`alisema Bw Rweyamamu kwa niaba ya Rais.Habari hii na Simon Mhina,Picha Mrocky

No comments: