Friday, April 25, 2008

Tunachunguza Shutuma za Mkapa- Pinda..


SERIKALI imesema inachunguza tuhuma zilizoibuliwa bungeni wiki hii na Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM) dhidi ya Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa,Pichani na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini,Daniel Yona kwamba walitumia vibaya ofisi za umma walipokuwa madarakani, kuanzisha kampuni binafsi kinyume cha sheria.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliliambia Bunge mjini Dodoma jana,kuwa serikali ina taarifa za tuhuma hizo,ambazo alisema zimeibuka kwa nguvu katika siku za hivi karibuni.


Kutokana na hali hiyo, alisema serikali inazichunguza ili kufahamu ukweli wa kilichotokea na kwamba, ikidhihirika na ushahidi ukapatikana, hatua zitachukuliwa kwa maslahi ya taifa.

“Suala hilo liliibuka kwa nguvu sana. Tunafuatilia kujua hali halisi ya kilichotokea. Taarifa za kutosha zikipatikana, tutafikia uamuzi utakaokuwa kwa maslahi ya nchi yetu,” alisema Pinda alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa papo kwa wabunge katika mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.Habari hii na Muhibu Said kutoka Dodoma

No comments: