Ziara ya Rais Kikwete Mkoani
Iringa...
Rais Jakaya Kikwete akimjulia hali mtoto Desderius Mrongo mwenye umri wa miaka miwili na nusu aliyelazwa katika Hospitali ya Consolata Ikonda,wilayani Makete.Aliyembeba mtoto Desderius ni nyanya yake ambaye alimweleza Rais kuwa mama mzazi wa mtoto huyo amefariki Dunia.Rais Kikwete yupo Mkoani iringa kwa Ziara ya kikazi kukagua na kufungua miradi ya maendeleo
Rais Jakaya Kikwete akiongea na watoto mapacha walioungana Maria na Consolata wakati alipotembelea Hospitali ya Kanisa Katoliki inayoendeshwa na wamissionari wa Shirika la Consolata iliyopo Ikonda Makete,Mkoa wa Iringa
Rais Jakaya Kikwete akiongea na watoto mapacha walioungana Maria na Consolata wakati alipotembelea Hospitali ya Kanisa Katoliki inayoendeshwa na wamissionari wa Shirika la Consolata iliyopo Ikonda Makete,Mkoa wa Iringa jana.Mapacha hao ambao sasa wana umri wa miaka kumi na moja( 11)hawawezi kutenganishwa kwa upasuaji kutokana sababu za kitaalamu, ni yatima ambao wazazi wao wamefariki kwa ugonjwa wa ukimwi lakini kwa bahati nzuri wao hawakuathirika na wanaendelea vizuri kiafya.Mapacha hao ambao wanahudumiwa na watawa wa Shirika la Consolata hivi sasa wanasoma darasa la tano katika shule ya Msingi Ikonda Makete na hivi sasa wanaishi nyumbani kwa Bi Betina Mbilinyi karibu na shule wanayosoma.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na watoto wa shule ya msingi Kilocha muda mfupi baada ya kuzindua ujenzi wa shule ya wasichana ya Anna Makinda jana.Picha zote Freddy Maro/Ikulu
No comments:
Post a Comment