Thursday, August 7, 2008

Ziara ya Rais Kikwete Isimani,
Iringa..


Mtoto Mkungile Tuasi(2)ambaye ni yatima akimuamkia Rais Jakaya Kikwete wakati Rais alipokizindua Rasmi kituo cha kulelea watoto yatima kinachojulikana kama Nyumbani kilichopo katika parokia ya kanisa Katoliki Isimani,mkoani Iringa jana.Pembeni aliyemshikilia mtoto huyo ni mhudumu wa kujitole wa kituo hicho kutoka India Maryammaa Thottukadavil.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mmissionari wa Shirika la kidini la Italia Lay association Maria Urzilia muda mfupi kabla ya Kufungua kituo cha watoto yatima kinachofadhiliwa na kuendeshwa na kanisa Katoliki eneo la Isimani
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya vijana voluntia Kutoka Italia waliojitolea kufanya kazi katika kituo cha kulelea watoto Yatima kilichopo katika Parokia ya Isimani.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Vodacom foundation Bi.Mwamvita Makamba(Kushoto) akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete hundi ya mfano ya milioni Thelathini kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wasichana katika shule ya sekondari Isimani.Hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika katika viwanja vya Isimani muda mfupi baada ya Rais kuhutubia mkutano wa hadhara.Kulia ni Mbunge wa Isimani ambaye pia ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh.William .Picha na Freddy Maro/Ikulu

No comments: