Serikali Yabadili Hati Za
Ardhi
---------
SERIKALI imebadili nyaraka za kumiliki ardhi na kutoa nyaraka mpya ili kukwepa utengenezaji wa nyaraka feki na kuimarisha usalama na uhakika wa miliki.
Hayo yalielezwa jana bungeni na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati, katika hotuba yake wakati akiwasilisha bungeni hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2008/09.
Chiligati, alisema hivi sasa wizara inaendelea na utaratibu wa kubadili nyaraka hizo na zile za zamani zinapaswa kuwasilishwa wizarani.
Aidha, alisema sera ya taifa ya ardhi, inatambua kuwa ardhi yote ni mali ya umma, hivyo mfumo wa kumiliki ardhi ni ule wa haki ya kutumia na si kuhodhi.

No comments:
Post a Comment