Sakata la Kifo Cha Chacha Wangwe:
Ndugu Hawajaridhika...
Ndugu Hawajaridhika...
Pichani ni Ndugu wa aliyekuwa mbunge wa Tarime marehemu Chacha Wangwe,Profesa Samuel Wangwe akisalimiana na Mwenyekiti wa Jukwa la wahariri Sakina Dattoo muda mfupi kabla ya kutangaza ripoti ya familia juu ya kifo cha marehemu nduguye,alipokutana na jukwaa la wahariri jijini Dar es Salaam leo
---------
Na Said Mwishehe.
Sakata la kifo cha Mbunge wa Tarime bado linaendelea, ndugu wa marehemu Wangwe bado hawajaridhika na maelezo ya jinsi ya ajali livyotokea na wanahisi ajali ilikuwa ya kupangwa.
Katika mazungumzo na waandishi wa habari,Prof Samuel Wangwe alitaja maswali yafuatayo ambayo yanahitaji majibu:
Kutokana na maswali hayo familia imesisitiza kuwa ajali hiyo inastahili ifanyiwe uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli. “Inawezekana kabisa si‘reckless driving(uendeshaji wa kizembe)’peke yake.”
Wanafamilia pia wameahidi kufuatilia na kushirikiana na polisi katika upelelezi huo ili kubaini ukweli wa chanzo cha ajali hiyo. Imewaomba raia wote wenye taarifa yoyote kuhusu uhusiano kati ya Malya na marehemu Chacha na wengine watoe habari kwa polisi ili kusaidia katika upelelezi huo.
Familia hiyo imesema kuwa uchunguzi uliofanywa na madaktari matokeo yake hayajatoka kwani inachukua muda kufanya uchambuzi kamili wa kile ambacho mtaalamu alikiona katika uchunguzi wa mwili wa marehemu.
Profesa Wangwe alisema familia inaamini kwamba matokeo hayo yakitolewa yatakuwa kielelezo kimojawapo katika vielelezo vitakavyotumiwa na polisi katika upelelezi wa kifo cha ndugu yao.
Wangwe alisema walilazimika kutoa taarifa kuwa mwili haukukutwa na risasi kwani kabla hata uchunguzi huo kukamilika tayari yalikuwepo maneno yaliyozagaa mjini Tarime kuwa alikutwa na risasi mbili kichwani.
Alisema katika hali hiyo wawakilishi wa familia waliamua kwamba ilikuwa vema kutoa tamko la awali kutokana na kile walichoshuhudia pale hospitalini Tarime ambapo uchunguzi wa mwili wa marehemu ulifanyika.

1.“Kwa nini Deus Mallya alianza urafiki na marehemu hivi karibuni ndani ya wiki tatu au
nne na urafiki huo ukawa karibu kwa haraka namna hiyo?
2.“Kwa nini Deus Mallya ndiye alikuwa anashinikiza hiyo safari ya usiku wakati watoto wa Chacha na mke wake walikuwa wanamshauri asisafiri siku hiyo usiku?
3.Ilikuwaje Deus ana shida na safari hiyo kuliko watu wengine wakiwemo marehemu mwenyewe na watoto wake na mke wake?
4.“Kwa nini hapo awali Deus hakutaka ajulikane kwamba yeye ndiye alikuwa anaendesha
gari hilo.
5."Kwa nini Deus hajaeleza kuhusu huyo mtu wa tatu aliyeonekana kuwa pamoja
na waliopata ajali?
6.“Kama huyo mtu wa tatu alitoweka baadaye kuonekana na waliofika katika eneo
la ajali alikuwa anakimbia nini?
7.Kwa nini Laptop ya Deus ambayo alikuwa anafanyia kazi zake nyingi ilitoweka baada ya ajali wakati simu na fedha zilikutwa katika eneo la ajali?
8.“Je ni kawaida wananchi wa kawaida kuona kwamba ni muhimu kuchukua Laptop kuliko kuchukua simu na fedha?
9.Kwa nini Deus alidai kwamba waliondoka Dodoma saa 9 mchana wakati familia yake inajua kwamba waliondoka baada ya saa 12 jioni?
10.Kwa nini Deus hakutaka ifahamike kwamba waliondoka usiku?

No comments:
Post a Comment