MAKALA YA LEO...
*Chetu ni chao na chao ni chao tu.
*Chetu ni chao na chao ni chao tu.
----------
Na Deus Ngowi.
HAYO yalitokea siku nyingi,nakumbuka,
Ningependa kurejea tena katika zahama ile,
Naam,kurejea zama zile chungu kwetu,
Kule kule: Tulikofuata njia ile ngumu
Kuzaliwa au kufa? Ni wazi palikuwapo uzao,
Hapana shaka, niliona kuzaliwa na kufa,
Lakini nikaona ni tofauti; kuzaliwa huko,
Mateso makali, kama kifo, ndio, kifo chetu,
Tulirejea makwetu, katika falme hizi,
Lakini mambo si rahisi tena, yameharibika,
Wageni wanashikamana na miungu wa kigeni,
Ningependelea mno kukiona kifo kingine.
Hayo ni maneno ya mwisho mwisho katika ‘Journey of the Magi’, kazi ya Thomas Stearns Eliot, maarufu zaidi kwa kifupi chake, T.S. Eliot, mwanafasihi mahiri wa enzi zake, aliyezaliwa Septemba 26, 1888 nchini Marekani. Alihamia Uingereza 1927, ambapo roho yake iliuacha mwili Januari 4, 1965. Alitunukiwa Nishani ya Nobel katika Fasihi 1948.
Huyu ameandika mashairi, kama vile The Love Song of J. Alfred Prufrock; The Waste Land; The Hollow Men; Ash Wednesday, na Four Quartets; ameandika michezo kama Murder in the Cathedral na The Cocktail Party. Kadhalika ana kazi yake iitwayo Tradition and the Individual Talent.
Nasi tunatakiwa tutamani tena kifo kingine, ili tukitoka, iwe imetoka (kama wasemavyo vijana wa mjini), si kurudia rudia sehemu moja kila wakati. Tutabaki tukicheza Sendema, ambayo wanaoijua wanasema ukienda mbele, nyuma, kushoto, kulia ni Sendema na hatimaye unabaki pale pale, lakini ukiwa mchovu kwa ‘kazi’ isiyokuwa na faida.
Pasipo kutumia mbinu alizotaka kutumia Rais wa Kwanza wa Ghana, Dk. Osagyefo Kwame Nkrumah kabla ya kuhujumiwa, Taifa letu halitakwamuliwa lilipo. Aliitwa Osagyefo na maana yake ni mshindi. Yeye, baada ya kuipatia Ghana Uhuru kutoka kwa Mwingereza, alilenga kuipaisha Ghana kiuchumi, lakini kwa mtindo ambao wengine waliona ni kama kuwapeleka kwenye kifo.
Mithili ya T. S. Eliot anavyoeleza walivyotembea katika machungu, baridi, miiba hadi kufika kwenye falme wanazoishi, na angependa warejee huko ili kupata ukombozi wa kudumu, Nkrumah naye alitaka wawe na mapinduzi ya viwanda na uzalishaji mkubwa zaidi.
Ni katika hali hiyo, aliamua kupunguza utegemezi katika mtaji kutoka nje, teknolojia na mali ghafi ili kweli Ghana iwe huru na kuepuka taifa la kichuuzi au uhuru wa bendera pasipo ule wa kiuchumi na kifikra. Kwa bahati mbaya, aliingiza gia ya mapinduzi ya viwanda mgongoni mwa wakulima wa kakao, zao lililoanza kuwa uti wa mgongo wa uchumi wa Ghana.
Yeye alitaka faida kubwa iliyopatikana irejeshwe kuwekezwa kwenye kilimo na nyingine kwenye ukuzaji uchumi, wananchi wakamwona msaliti. Hatima yake ilikuwa kukwama kwa miradi kadhaa ya kiuchumi aliyoanzisha, likiwamo Bwawa la Akosombo ambalo lingegharimu kiasi kikubwa cha fedha. Hata hivyo, leo linatumika, lakini yeye alitaka kwenda mbali zaidi. Hadi anaangushwa madarakani 1966, Ghana ilishayumba kiuchumi.
Wananchi, wakiongozwa na wachache wenye uchu wa faida ya haraka na wenyewe kula matunda badala ya vizazi vyao, walimkatalia kuwekeza tena faida ya mauzo ya bidhaa za wananchi wa Ghana ili kunyanyua uchumi katika sekta zote. Nasi tusipoona mbali hatutaweza ‘kutoka’. Naam, hatutaweza kufufuka baada ya kifo, kwa sababu wanasema hujafa hujaumbika.
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye alipata kuzungumzia akipinga dhana ya vijana kukimbilia mijini halafu wakawa wanauza “soksi moja mtaani”, badala ya kushiriki katika kazi za uzalishaji. Alisema hayo akiwa madarakani katika Serikali ya Awamu ya Tatu. Alikuwa sahihi, lakini baadhi ya wamachinga walimdhihaki, wakisema mbona yeye aliondoka kwao akaja jijini Dar es Salaam. Lakini yeye hauzi soksi moja!
Ukweli ni kwamba, maneno yake yana maana kubwa ambayo isipozingatiwa, letu litakuwa Taifa la wachuuzi, ambalo ni hatari na haliwezi kusimama imara katika myumbo wa biashara shindani na huria, zisizokuwa na huruma kwa wanyonge na zenye kumpendelea mwenye kutumia akili, na kwa hakika mwenye kuzalisha kwa wingi na kwa teknolojia ya hali ya juu.
Maneno ya Eliot katika kitabu chake hicho, ni onyo kwetu na kwa walio wetu na ni changamoto ya kutoogopa matatizo au magumu ya maisha, kwa sababu hakuna waridi pasipo miiba, wala hakuna aliyepata kuishi hapa duniani, akawa raha mustarehe tangu kuzaliwa hata kifo chake.
Kwa maneno mengine, ni kwamba lazima tukubali hujafa hujaumbika. Pia kwamba daima maisha ni kujifunza kila hatua, kuweka juhudi na kuendeleza taasisi za uzalishaji, kwa maana watu huja na kupita lakini tangu kuumbwa dunia hadi leo, taasisi na mataifa yanaendelea, hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo na aliyeviumba.
Sisi baada ya kudharaua mwiba, kuota matende na matende yenyewe kuanza kutuelemea, lazima tuangalie njia ya kuondokana nayo, maana tunayumba kutokana na uzito wake na sababu nyingine zitokanazo nayo.
Tunapoyumba jinsi hii, wenzetu wasiotutakia mema wanachekea chooni, maadui wanafurahi kwa sababu kuvuja kwa pakacha ni nafuu kwa mchukuzi, maana yake ni kwamba anapungukiwa uzito, anabeba bila shida, kwa hiyo anaepuka ‘mateso bila chuki’ tunayojitakia wakati mwingine.
Alisema mwakilishi mmoja wa wananchi wiki iliyopita, kwamba mwaka 1974 njaa ilipotokea nchini, Watanzania walijifunza baada ya baa la njaa, kwa sababu vyombo vyetu vimekuwa vikiwaendekeza katika kuelimishwa wakati majanga yanatokea kuliko kuwaelimisha jinsi ya kuondokana na matatizo hayo.
Kwa vigezo vyovyote vile, Tanzania wala Zimbabwe hazikuwa nchi za kulia njaa.
Kadhalika nchi nyingine nyingi katika ukanda wetu. Lakini kwa kuwa upendo huanzia nyumbani, tutabaki tukishangaa na kusoma hotuba za kihistoria hadi lini kuhusu mambo ya kilimo? Kwamba kuna mkakati kabambe, kuna mapinduzi makubwa, yanakuja mageuzi ya kijani, maofisa ugani wanarudi hadi vijijini. Lini?
Dunia si yetu wala hatuna miadi nayo, makataa yanaweza kutolewa muda wowote, na tuendako tutahukumiwa kwa hotuba na kujidai kwetu na mipango mizuri inayobuniwa na kuhifadhiwa (labda kwa ajili ya kizazi kijacho). Kweli walalahoi au wanyonge, watu wa mafigani warudie tena kula yanga la kupangia foleni kutoka kwa Mwamerika? Vyuo na wasomi wetu wote wanafanya nini?
Inasikitisha kuona kwamba wengi waliofunzwa kilimo na ufugaji sasa wapo kwenye sekta nyingine tofauti, baadhi katika uandishi wa kisiasa, benki, ubunge na hata wengine kukimbilia kuongeza stashahada ya juu na kubobea kwenye sekta nyingine, wakikiacha kilimo na mifugo kama yatima.
Na hii sababu yake inajulikana, hakuna kichocheo cha wao kuwa huko kwenye kilimo na ufugaji, hawawezi kwenda kuishi Bukombe, Nanyamba wala Kibaya kwa mshahara au posho ya ajabu kiasi hicho wakati wanaopiga siasa wanapata mamilioni. Hatutoki kwa jinsi hii.
Lakini pia, sasa katika kukuza msemo wa chetu ni chao na chao ni chao, tunaona utitiri wa wageni, pengine baadhi wakiwa hawana hata sifa wala vigezo katika taaluma husika, wakiwa walimu kwenye shule zetu, wakiwa wataalamu kwenye kampuni na wakiwekwa juu ya Watanzania waliosoma zaidi na wenye ujuzi zaidi na mazoea ya nchi yetu.
Kama ndivyo, kwa nini wataalamu wasikimbilie siasa ambako wageni hawaruhusiwi? Tuombe tu kwamba katika kufungua milango siku moja wageni hawataruhusiwa kuingia kwenye mabaraza ya udiwani, uwakilishi na ubunge!
Lipwoto wabaya wapo macho wakitaka kutuharibia, na katika mkato wa tama wa watu wetu, labda wakitaka tuyaone maisha katika ‘mwanga mpya’, wamekuja na mambo mapya pia. Nayo ni utitiri wa madhehenu ya dini, yenye majina ya ajabu kabisa, wengine wakijiita ni kanisa la mwisho kabisa, wakija na kuanzisha shule zao na walimu wa Kizungu, wanaobaki wanaombewa kwenye sekondari zetu. Kwa kuwa tunatetemeka, tunawaruhusu na kuwapa vyeo, wanafunzi wetu wakifurahi kwamba wanaye mwalimu au wanao walimu Wazungu, wenye kila aina ya uchawi wa elimu na waliotoka kule ambako “hatimaye elimu hufika mwisho.”
Nani alipata kuona mwisho wa bahari au mbingu? Wazungu na wageni wengine wanaotumia mbinu hizi, si kwamba wamesoma sana, bali ni wasanii wa kucheza na mazingira na akili za watu. Ndio maana wanaona kwa kuwa huko kwao kazi zimeisha, maisha yanabadilika kwa kasi na maeneo yao ni madogo kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda au kilimo, wanawaleta huku kama kwenye dampo kama wafanyavyo kwa bidhaa zao zisizokuwa na kiwango, lakini ambazo huruhusiwa tu kuingia, kwa sababu zinazojukikana zaidi na wataalamu wetu tuliowapa kazi ya kudhibiti pamoja na mamlaka zilizo juu yao.
Ukiuliza hayo, wanasiasa wetu watasema kila jitihada zinafanyika katika kuzuia hali hiyo, akiapia mbingu kwamba anafuatilia suala hilo kwa juhudi, wakati akiwa hajui na hata baadhi ya majibu anapata kwa ‘vimemo’ kutoka kwa wataalamu waliokaa mbali kidogo naye, lengo likiwa ni ili hoja yao ipite tu mbele ya wawakilishi wa watu. Tumefikia kuwauza watu wetu? Kuwaacha wafe kwa dawa feki na vyakula vilivyooza lakini vinavyonukia kwa sababu hao wa ng’ambo wamevipulizia aina ya marashi wanayoyajua wenyewe?
Turejeshe kwa asilimia 100 udhibiti wa mali zetu na wageni uchwara wanaokuja kwa jina la dini mpya, zinazolenga kusambaratisha umoja na mshikamano wetu, kutibua ukweli wa mambo kwa maana ya ukweli, kwa kubadilisha uongo kuwa ukweli na ukweli kuwa uongo. Tuna kila kitu lakini tunakaribia kushindwa kila kitu kwa ajili ya kila mtu wetu kila wakati.
Mola tunusuru na matende haya tukomboe kilicho chetu. Naam, hatuwezi kufikia huko pasipo kukubali na kukipokea kifo kipya. Hata lini chetu kibaki kuwa chao, lakini chao kadhalika kisiwe chetu na kubaki kwao? Ningependelea kifo hicho kingine, ili kitukwamue moja kwa moja.

No comments:
Post a Comment