Wednesday, August 13, 2008

Madaktari Muhimbili Wasitisha
Mgomo...

Madaktari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,wakiwa katika mavazi ya kawaida katika maeneo ya hospitali hiyo jijini Dar es Salaam jana.Mgomo huo, jana uliingia katika siku ya tano katika kushinikiza nyongeza za posho.Picha na Mdau Yusuf Badi/TSN.
------------
*Watoa masharti ya kurejea kazini
*Serikali kuwaadhibu watakaoendelea
*TUCTA yatangaza mgomo wa siku tatu
MADAKTARI walioko mafunzoni katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH)wamesitisha mgomo wao jana na kurejea kazini kwa muda wa siku saba,hadi pale uongozi wa hospitali hiyo utakapotekeleza madai yao kamili ifikapo Jumatatu ijayo.Wakati wakichukua hatua hiyo, serikali imewaagiza madaktari wote waliogoma warudi kazini mara moja kuendelea na kazi na wasipofanya hivyo hatua kali za kinidhamu dhidi yao zitachukuliwa.Bofya na Endela....>>>>>

No comments: