Wednesday, August 20, 2008

Msiwatoze Wanajeshi Nauli
-Dr Mwinyi


---Pichani ni Waziri wa Ulinzi na jeshi la Kujengwa Taifa Dr Hussein Mwinyi

Msimbe Lukwangule.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka wamiliki wa daladala wasiwatoze nauli askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ)wakati mazungumzo ya kutafuta mwafaka juu ya suala hilo yakifanyika.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa majumuisho ya mjadala wa makadirio ya matumizi ya wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga Taifa.Kwa mujibu wa Dk.Mwinyi,hivi sasa yanafanyika mazungumzo kati ya wizara yake,Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(Sumatra)na wamiliki wa daladala kuhusu suala hilo la ulipaji nauli na baadaye itatolewa kauli rasmi.

“Kwa kuwa wamiliki walishawachukua (askari) kwa miaka mingi tunaomba waendelee kwa utaratibu huo wa zamani hadi hapo utaratibu mpya utakapotangazwa,”alisema Dk.Mwinyi bila kufafanua.Julai 31,mwaka huu,gazeti la HabariLeo iliripoti ikimnukuu Msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Meja Jenerali Alfred Mbowe akisema waraka ulikuwa umesambazwa ukiwataka wanajeshi wote wanaotumia usafiri wa daladala kulipa nauli kuanzia Agosti mosi hata kama watakuwa wamevaa sare.

1 comment:

Anonymous said...

kusema ukweli namuuuuunga mkono Mh.WAZIRI na kupinga maneno ya msemaji wa jeshi coz askari yuko kazini mda wote sasa ikitokea dharura ikatakiwa apande mabasi hata matatu hamwoni at the end ukilinganisha mshahara wake ni sawa na nauli alizotumia kwa mwezi mzima.
Huo mfumo unaotaka kuanzishwa si sahihiata kidogo,kama msemaji wa jeshi anasema askari wake walipe nauli kwa kua tu hajui wanahangaika vp kwa kua wao hutembelea difenda mda wote.
Ila huo ni mwono wake na mimi km raia ni mwono wangu,km inawezekana serikali iwatafutie askari wetu usafiri wao ambao hawatajimix na raia wengine.